Kamishna
Jenerali Wa Uhamiaji kwa niaba ya Watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji Tanzania
anawatakia Watanzania Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya wa 2018.
Aidha
anatoa wito kwa wananchi wote hasa waishio maeneo ya mipakani kutoa taarifa kwa
Idara ya Uhamiaji ama Vyombo vingine vya Dola pale wanapoona makundi ya watu
wakipita katika maeneo yao, kwani Wahamiaji Haramu wanaweza kujipenyeza na
kuingia nchini kipindi hiki cha Sikukuu za Mwisho wa Mwaka.
Pia
anawakumbusha Watanzania kuwa, Uvushaji, ama Usafirishaji, Uhifadhi wa
Wahamiaji Haramu au Usaidizi wa aina yoyote
kwa Wahamiaji ni Kosa la Jinai kwa Mujibu wa Sheria ya Uhamiaji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni