Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu amefanya ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 18-19 Disemba 2017 katika Mkoa wa
Kusini Pemba, ikiwa ni muendelezo wa ziara za kukagua utendaji kazi wa maafisa
uhamiaji ili kuhakikisha wananchi na wageni wanapata huduma kwa wakati.
Akiwa
katika Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Mkoani, alikagua vitabu vya Hati za
kusafiria zinazotolewa kwa Watanzania wanaohitaji kusafiri nje ya Nchi na kuwasisitiza
Maofisa Uhamiaji katika utoaji wa Hati hizo wazingatie vyema Sheria na Taratibu
zilizopo ili kuepusha matumizi yasiyo sahihi.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu aliwanasihi Maafisa, Askari na watumishi
Raia wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba kuzingatia maadili ya kazi,
pamoja na kutilia mkazo matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.
“Naelewa
tupo kwenye utandawazi, lakini narudia kuwasihi matumizi ya Mitandao ya kijamii
itumike kwa kuzingatia Kanuni na Miongozo ya Serikali, pia mjiepushe na utoaji
wa Siri na Taarifa za serikali, ni mwiko kutoa taarifa yoyote, fuateni Sheria
na Taratibu tulizowekewa.” alisema Kamishna Sururu.
Mkaguzi
Msaidizi wa Uhamiaji, Juma A. Khamis alipokuwa akichangia hoja wakati wa kikao
cha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji walioko
Mkoa wa Kusini Pemba siku ya tarehe 19 Disemba, 2017. Alisema “Ongezeko
la Bandari Bubu ndani ya Wilaya ya Mkoani ni changamoto kubwa katika
utekelezaji wa majukumu yetu. Tunazo takriban Bandari bubu 103, tunaomba Idara
itupatie gari la kufanyia doria katika maeneo hayo”. Kwa upande wake
Kamishna Sururu aliahidi
kulifanyia kazi ombi mapema iwezekanavyo.
Katika
ziara hiyo, Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu ambaye aliambatana na
Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, alikagua baadhi ya bandari
Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini Magharibi
mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii, ambazo
hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo kinyume na
taratibu za Uhamiaji.
 |
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M.
Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua
baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia ya Kengeja, Kusini
Magharibi mwa kisiwa cha Pemba.
|
 |
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu
(kushoto) akikagua baadhi ya magari chakavu yaliyopo katika Ofisi ya Uhamiaji
Mkoa wa Kusini Pemba, yanayosubiri kupigwa mnada baada ya kukamilika kwa
taratibu za uuzaji wa Mali za Serikali, wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa
Kusini Pemba tarehe 18 – 19 Disemba, 2017. Pamoja na kutembelea maeneo mbali
mbali ya utendaji kazi Mkoani humo ikiwemo Bandari ya Mkoani, Bandari ya Wesha
iliyopo Chake Chake na Bandari bubu kadhaa. Kulia kwake ni Afisa Uhamiaji Mkoa
wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdi Bulushi.
|
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Hassan A.
Ramadhan (kulia) akifafanua jambo kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M.
Sururu (wa pili kulia) kuhusu mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
inavyosaidia kurahisisha mawasiliano na utendajikazi katika Ofisi ya Uhamiaji
Mkoa wa Kusini Pemba.
 |
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Juma A. Khamis
(aliesimama) akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,
Johari M. Sururu (hayupo pichani) na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji walioko
Mkoa wa Kusini Pemba siku ya tarehe 19 Disemba, 2017
|
 |
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M.
Sururu akikagua kitabu cha utoaji wa Hati za Dharura za Kusafiria “ETD” katika
Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Mkoani, zinazotolewa kwa Watanzania wanaohitaji
kusafiri nje ya Nchi.
|
 |
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M.
Sururu akitoa nasaha zake kwa Maafisa, Askari na watumishi Raia wa Idara ya
Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, wakati akihitimisha ziara ya kikazi Mkoani humo
Leo tarehe 19 Disemba, 2017.
|
 |
Sheha wa Shehia ya Kengeja, Mohamed Kassim
Mohamed (kulia) akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu
(katikati) na Maafisa waandamizi wa Uhamiaji alioambatana nao, Bandari bubu ya
Mbuyuni inayotumiwa na wananchi wa eneo hilo kwa mahitaji mbali mbali ikiwemo
uvuvi.
|
 |
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M.
Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua
baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia ya Muwambe, Kusini
Magharibi mwa kisiwa cha Pemba.
|
 |
Mkaguzi Msaidizi
wa Uhamiaji, Hassan A. Ramadhan (kulia) akifafanua jambo kwa Kamishna wa
Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kulia) kuhusu mifumo ya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano inavyosaidia kurahisisha mawasiliano na utendajikazi
katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba.
|
 |
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu
Kamishna wa Uhamiaji, Abdi Bulushi akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,
Johari M. Sururu (wa pili kulia) na Maafisa Uhamiaji aliombatana nao, matunzo
na usafi wa mazingira katika nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, zilizoko
eneo la Ndugukitu, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba.
|
 |
Nyumba za makazi ya Askari na Maafisa Uhamiaji zilizopo Ndugukitu Chakechake zilifunguliwa rasmi na Mhe. Makamo wa Pili
wa Rais, Balozi Seif Iddi mapema mwezi Januari, 2017.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni