Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Dkt Anna Peter Makakala leo ameongoza Ujumbe wa Mabalozi
kumi na mbili katika Mafunzo ya huduma mbalimbali za kiuhamiaji zinazotolewa
katika Balozi za Tanzania Nje ya Nchi. Mabalozi hao wameteuliwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli hivi karibuni.
Katika
mafunzo hayo, mada mbalimbali ziliweza kuwasilishwa na Maafisa kutoka Idara ya
uhamiaji hususan Pasipoti, Visa za kielektroniki, Huduma za kibalozi (Consular
Services) pamoja na Mifumo inayotumika katika utoaji wa Pasipoti na visa za
kieletroniki.
Aidha,
Waheshimiwa mabalozi walipata fursa ya kutembelea na kujionea namna mifumo
mbalimbali ya Uhamiaji inavyofanya kazi na kuonyesha kufurahishwa na jinsi
mifumo hiyo inavyorahisisha utoaji wa huduma za uhamiaji kwa haraka na kwa
ufanisi mkubwa.
Kwa
upande wake Balozi wa Tanzania Nchini Kuwait, Mheshimiwa Aisha S. Amour kwa
niaba ya mabalozi wenzake alimshukuru na Kumpongeza Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji kwa mafunzo waliyoyapata. Pia ameongeza kuwa, mafunzo hayo
yatawajengea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi hususani katika kuwahudumia Watanzania
waishio nje ya nchi na wageni wanaoingia hapa nchini kwa madhumuni mbalimbali ikiwemo
utalii, matembezi, Biashara na uwekezaji.
Baadhi
ya waheshimiwa Mabalozi waliohudhuria
mafunzo hayo ni pamoja na Maj Gen, Gaudence Milanzi, Mohamed A. Mtonga, H.A Kattanga,
Aisha S. Amour, Prof. Emmanuel D. Mbennah, Ali J.Mwadini, Dkt. Jilly E. Maleko pamoja na Dkt.
Modestus F. Kipilimba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni