Afisa Uhamiaji ‘Feki’ Bushiri Ally Nassoro mwenye
umri wa miaka 19 leo tarehe 18 Novemba 2019, amekamatwa na Maafisa
Uhamiaji kwa tuhuma za kuwatapeli na kuwalaghai wateja wanaokuja kupata huduma
za Kiuhamiaji katika ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Kurasini jijini Dar es
salaam.
Katika mahojiano ya awali, Afisa huyo Feki pia aligundulika kudanganya kama Afisa Usalama wa Taifa. Kijana
huyo tapeli ambaye anadai ameanza kulaghai wateja tangu mwaka 2017 bado
anaendelea kushikiliwa na kuhojiwa kwa uchunguzi zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni