Kamishna wa Uhamiaji (Vibali na Pasi), Mary Palmer akiongea wakati wa mkutano huo. |
Kamishna Palmer akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Uraia na Masuala ya Uhamiaji wa Uganda Meja Jenerali Apollo Kassita-Gowa mara bada ya mkutano huo. |
Kamishna wa Uhamiaji Mary Palmer (ndc), anayesimamia Divisheni ya Vibali, Pasi na Visa, aliongoza
ujumbe wa Idara ya Uhamiaji Tanzania katika Mkutano wa Wakuu wa Idara za Uhamiaji
na Kazi za Tanzania na Uganda uliofanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es
salaam.
Lengo
la mkutano huo ni kuzikutanisha nchi za Tanzania na Uganda ili kujadili na kuzitafutia ufumbuzi
changamoto mbalimbali hususan za
kiuhamiaji zilizopo baina ya nchi hizo.
Katika
Mkutano huo, Kamishna Palmer alimuwakilisha Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt
Anna Peter Makakala, ambaye yuko nje ya Ofisi kwa majukumu mengine ya kikazi. Aidha,
ujumbe kutoka Uganda uliongozwa na Meja Jenerali Apollo Kasiita-Gowa, ambaye
pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Uraia na Masuala ya Kiuhamiaji nchini Uganda.
Akizungumza
wakati wa mkutano huo Kamishna Palmer alisema, ushirikiano baina ya nchi hizo
mbili ni muhimu sana katika kuimarisha udhibiti wa masuala mbalimbali ya
kiuhamiaji. Pia aliongeza kusema kuwa mkutano huo utasaidia kuongeza kasi ya
kuondoa vikwazo vya safari baina ya raia wa nchi za Tanzania na Uganda.
Kwa
upande wake Meja Jenerali Apollo Kasiita -Gowa akieleza umuhimu wa mkutano huo
alisema, sio tu utakuwa ni chachu katika kuongeza mtangamano na mshikamano
baina ya wananchi wa pande zote mbili bali pia utasaidia katika kurahisisha
taratibu za kiuhamiaji baina ya raia wa nchi mbii hizo, pamojana kuimamarisha
udhibiti wa uhalifu unaovuka mipaka (Transanational Crimes).
Mkutano
huo ni mwendelezo wa Mkutano wa tatu wa Wakuu wa Idara za Uhamiaji na Kazi baina
ya nchi za Tanzania na Uganda uliofanyika jijini Kampala, Uganda mwezi Novemba mwaka
jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni