Maafisa
Uhamiaji wanaosimamia doria na misako wameonekana maeneo mbali mbali ndani na
nje ya mji wa Singida wakitekeleza majukumu yao. Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji
Elizabeth Kichonge ambaye alikuwa akiongoza kikosi cha Maafisa na askari watano
alionekana akikagua nyaraka za wageni katika stendi ya mabasi ya mikoani mjini Singida.
“Kutokana
na wimbi la wahamiaji haramu kubadili njia na sasa kupitia Mkoani kwetu kuelekea
kusini mwa nchi, tumeamua kuzidisha ukaguzi kwenye vyombo vya usafiri. Kupitia
zoezi hili, kuna mafanikio ambayo tumeyaona; mfano kwa siku chache hizi
tulizofanya kazi, tumeshakamata watuhumiwa zaidi ya thelathini” Alisema Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Angela Shija ambaye
ni Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Singida.
Pamoja
na ukaguzi, doria na misako inayoendelea kwa sasa, pia Uhamiaji Mkoa wa Singida
wanatoa elimu ya Uhamiaji na Uraia kwa abiria wa mabasi, wananchi wa kawaida pamoja
na vijana wanaoshiriki mafunzo ya Mgambo Mkoani humo. Pia Idara ya Uhamiaji Mkoani
Singida inashirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
katika kufanikisha zoezi la uandikishwaji wa vitambulisho vya Taifa ili
kuhakikisha watu wasiostahili hawajipenyezi kwa lengo la kuandikishwa.
Hadi
sasa wahamiaji haramu 30 kutoka nchi za Maziwa Makuu (Rwanda, Burundi na DRC)
tayari wameshakamatwa na hatua mbalimbali zimechukuliwa dhidi yao ambapo watu
watano wamehalalisha ukaazi wao nchini, watu saba wameondoshwa nchini, watu 17
wanaendelea kuchunguzwa uhalali wa uwepo wao nchini na mmoja alifikishwa
mahakamani na kukutwa na hatia ambapo alifungwa jela mwaka mmoja.
![]() |
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Elizabeth Kichonge akikagua
nyaraka za wageni katika stendi kuu ya mabasi yaendayo Mikoani.
|
![]() |
Koplo wa Uhamiaji Faraja Wanjara akitoa elimu ya Uhamiaji na Uraia kwa abiria
|
![]() |
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Isack Maganga (mwenye shati la draft) na
Koplo wa Uhamiaji Abdallah Makacha wakiwateremsha watuhumiwa wa uhamiaji kwenye basi mara baada ya ukaguzi.
|
![]() |
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Lawi Kumburu akimchukua maelezo mtuhumiwa
alioingia nchini bila kibali cha Uhamiaji
|
![]() |
Afisa Uhamiaji akipekua begi la mtuhumiwa |
![]() |
Mkaguzi wa Uhamiaji Owden Kalengo na Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Lawi Kumburu wakimuhoji mtuhumiwa ili kujiridhisha juu ya uraia wake.
|
![]() |
Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Roman Mtono akitoa elimu ya maswala ya
Uhamiaji kwa vijana wanaoshiriki mafunzo
ya awali ya Mgambo.
|
![]() |
Wahamiaji Haramu waliokamatwa katika kizuizi cha barabara kuu iendayo Dar Es
Salaam
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni