Na Konstebo Amani Mbwaga, Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Mhe. Samia Suluhu Hassan amewatunuku Nishani Maofisa na Askari wa Uhamiaji 25 ikiwa ni historia kwa mara ya kwanza kutokea tangu Uhuru.
Akitoa salamu wakati wa hafla ya uvalishaji nishani kwa maafisa na askari hao Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala alianza kwa kumshukuru Mungu na kisha kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusaini sheria ya kuifanya uhamiaji kuwa Jeshi na hatimae kustahili kupata nishani ambazo zimekuwa zikitolewa kwa majeshi mengine kwa muda mrefu.
“Kwa mantiki hiyo hafla hii ni ya kwanza katika historia ya Jeshi letu hivyo tuna sababu ya kushukuru na kuenzi tunu hii” alisema Dkt. Makakala
Aidha Kamishna Jenerali Dkt. Anna Makakala amewapongeza maafisa na askari waliovalishwa nishani ambapo kimsingi zimetolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo yeye kama mkuu wa chombo cha ulinzi na usalama kwa mamlaka aliyokasimishwa na Rais chini ya kifungu cha 9 (1) cha sheria ya Uhamiaji sura 54 ikisomwa pamoja na kanuni ya 156 (2) ya kanuni za uendeshaji za uhamiaji amewavalisha kwa niaba yake.
Akihitimisha hotuba yake Dkt. Makakala alisema kwa uzito wa tunu waliyopatiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyonayo chini ya kanuni ya 156 (1) ya kanuni za uendeshaji za Uhamiaji za mwaka 2018 inatupasa maofisa na askari kuzitendea haki kwa kuwajibika zaidi na kutekeleza majukumu kwa weledi, ari na uadilifu wa hali ya juu sanjari na kuzingatia sheria, kanuni taratibu na miongozo inayosimamia kazi za uhamiaji.
Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru ilitolewa kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala ambae alivishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 09 Disemba 2021 wakati wa kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru, wengine ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu ambae alivishwa na Kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini kwa niaba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu sanjari na Naibu Kamishna wa Uhamiaji Albert Rwelamila, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Nasra Juma Mohamed na Mrakibu wa Uhamiaji Issa Mlweta Issa.
Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema ilitolewa kwa Mkaguzi wa Uhamiaji Kanyakula Titus Mrefu, Mkaguzi Wing Mombaka Said, Mkaguzi Hermina Azza Foya, Mkaguzi Emma Alex Kalyembe, Mkaguzi Beatrice Elineema Nyange, Mkaguzi Dkt. Clement Bernado Mubanga, Mkaguzi Othman Khamis Ali, Mkaguzi Fikirini Abdallah Ali, Mkaguzi ABubakary Muhozi Yunusu, Mkaguzi Pilli Ally Mazige, Mkaguzi Msaidizi Gloria Godfrey Shayo, Mkaguzi Msaidizi Jane Deusdedit Luhaga, Mkaguzi Msaidizi Zahra Abdu Akida, Mkaguzi Msaidizi Salma Mahboob Mkadar, Stafu Sajini Mbaraka Yusuph Ayoub, Stafu Sajini Bahati Jamali Ramadhani, Stafu Sajini Seif Abdullatif Khamis, Stafu Sajini Juma Omar Suleiman, Sajini Nyambeho John Siwa na Konstebo Stephano Aram Kayaga.
HABARI PICHA NA MATUKIO
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru Naibu Kamishna wa Uhamiaji Nasra Juma Mohamed katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru Naibu Kamishna wa Uhamiaji Albert Rwelamila katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru Mrakibu wa Uhamiaji Issa Mlweta Issa katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akitoa Nasaha na Maelekezo kwa Maafisa Askari na Watumishi raia wa Uhamiaji mara baada ya kutunuku Nishani katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam |
|
Mkuu wa Kitengo cha Utumishi Uhamiaji Makao Makuu ACI James Mwanjotile akitoa maelezo mafupi kuhusu Nishani wakati wa hafla ya uvalishwaji Kurasini Jijini Dar es salaam |
|
Kamishna wa Uhamiaji Fedha na Utawala Hamza Shabani |
|
Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Pasipoti na Uraia Gerald Kihinga (Kulia) |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akizungumza na vyombo vya habari baada ya hafla ya kuvisha Nishani kwa Maofisa na Askari wa Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam |
|
Picha ya Pamoja Maofisa na Askari |
|
Picha ya Pamoja na Brass Band ya Polisi |
|
Picha ya Pamoja na Uhamiaji Tanzania Band |
|
Picha ya Pamoja na NCOs waliovishwa Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Konstebo wa Uhamiaji Stephano Aram Kayanga katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Sajini Nyambeho John Siwa katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Stafu Sajini Seif Abdulatif Khamis katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam
|
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Stafu Sajini Bahati Jamali Ramadhani katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam
|
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Stafu Sajini Mbaraka Yusuph Ayoub katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Mkaguzi Msaidizi Salma Mahboob Mkadar katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Mkaguzi Msaidizi Zahra Abdu Akida katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Mkaguzi wa Uhamiaji Pili Ally Mazige katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam
|
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Mkaguzi wa Uhamiaji Dkt. Clement Bernado Mubanga katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam
|
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Mkaguzi wa Uhamiaji Beatrice Elineema Nyange katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam
|
|
Mfawidhi Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl, Nyerere (JNIA) Naibu Kamishna wa Uhamiaji Albert Rwelamila akiteta jambo na Msemaji Mkuu wa Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle wakati wa hafla ya uvalishaji wa Nishani iliyofanyika Kurasini Jijini Dar es salaam (Picha zote na Konstebo Amani Mbwaga Uhamiaji Makao Makuu) |
kazi nzuri constable Amani Mbwaga big up
JibuFuta