Maafisa Uhamiaji 15 waliokwenda nchini China kwenye ziara ya
mafunzo ya wiki mbili wamerejea nchini jana usiku wakitokea katika jiji la ShangChuan ambapo walipokelewa
na Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Ignasio Gunda Mgana.
Msafara
huo ulifika Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar leo majira ya saa tatu
asubuhi na kulakiwa na Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Hannelore Manyanga
ambaye alipokea taarifa ya safari na mafunzo.
Mrakibu
Mwandamizi wa Uhamiaji Mariam Mwanzalima ambaye ndiye kiongozi wa msafara huo
alieleza namna walivyosafiri na kupokelewa na uongozi wa chuo cha Uhamiaji
jimbo la ShangChuan na mafunzo waliyopata.
“Tunamshukuru Mwenyeezi
Mungu kutuwezesha kwenda na kurudi salama, Afande naomba ufahamu kuwa wale
wenzetu wa China walitupokea na kutukirimu sana. Mafunzo tuliyopata ndani ya
wiki mbili hizo ni masuala ya Human trafficking, border management issues,
smuggling, cybercrime, customer care na travel documents verification. Kwa
kweli tumejifunza mambo mengi ambayo yametufungua na yatatusaidia sana katika
utendaji kazi wetu wa kila siku, asante afande kwa kutuchagua kuiwakilisha
idara katika mafunzo haya’’ alieleza Mwanzalima.
Naye Kaimu Kamishna wa Jenerali wa Uhamiaji Hannelore Manyanga
aliwataka maafisa hao kutumia ujuzi waliopata katika mafunzo hayo ili kuboresha
huduma za uhamiaji na kupunguza
malalamiko kutoka kwa wananchi wanaofika kwenye ofisi za uhamiaji.
|
Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mariam Mwanzalima akimweleza Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Hannelore Manyanga juu ya safari yao ya China na Mafunzo waliyopata. |
|
Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Ignas Gunda Mgana (kushoto) akisikiliza kwa makini taarifa ya safari ya maafisa walikwenda nchini kwenye mafunzo ya wiki mbili |
|
Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mariam Mwanzalima akitoa taarifa ya safari ya mafunzo nchini China |
|
Kaimu Kamishna wa Uhamiaji Hannelore Manyanga akipokea zawadi ya Ngao ya Urafiki na Ushirikiano baina ya Tanzania na Idara ya Uhamiaji na Polisi ya China |
|
Picha ya pamoja wa maafisa walio rejea kutoka nchini China na Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (aliyekaa). |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni