Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Maj. Gen. Projest Rwegasira aliwaasa
Watumishi wa Idara ya Uhamiaji kufanya kazi kwa weledi na nidhamu.
Akizungumza na Watumishi hao kwenye Mkutano huo uliofanyika jana
TRITA Moshi Katibu Mkuu aliongeza kuwa Viongozi wa Idara ya Uhamiaji na
Watumishi wengine watumie Mkutano huo kutathmini mafanikio na changamoto
mbalimbali zinazokwamisha utendaji kazi wa Idara.
"Natambua kuwa vikao vya aina hii vipo kwa mujibu wa Sheria,
lakini pia ni muhimu sana kwa watumishi wa Kada ya kiraia ambao wanafanya kazi
katika Vyombo ambavyo mfumo wake wa uendeshaji ni wa kijeshi zaidi wakapata
fursa ya kusikilizwa hoja zao, kwani ipo dhana miongoni mwa watumishi raia kuwa
hawapati fursa ya kushiriki na kufahamu baadhi ya mambo muhimu yanayohusu
maslahi yao katika Vyombo hivyo. Mimi naamini Baraza hili ni uwanja mzuri sana
na uliowazi katika kujadili masuala mbalimbali yanayo gusa maslahi ya mtumishi
pamoja na mwajiri wake mahala Pa Kazi. Hivyo muutumie vizuri uwanja huu kwa
maslahi ya pande zote mbili" alisema Katibu Mkuu.
Hili ni Baraza kubwa la Kitaifa la Watumishi wa Idara ya Uhamiaji
Tanzania TUGHE ambalo hufanyika kila mwaka likiwa na lengo la kutathmini
utendaji kazi na kushughulikia maslahi ya Watumishi wa Kada ya Kiraia.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
(Mwenyekiti), Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar (Makamu Mwenyekiti), Makamishna wa
Uhamiaji wa Divisheni za Fedha na Utawala, Pasipoti na Uraia,
Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka, Viza na Pasi, Vibali vya Ukaazi na Wafawidhi
wa Vitengo toka Uhamiaji Makao Makuu na Zanzibar.
Kadhalika Viongozi wa TUGHE tawi la Uhamiaji Bw. Shaame A. Hamad
(Mwenyekiti), Triphonia J. Kimaro (Katibu), Eng. Amani Msuya (Naibu Katibu
TUGHE - Taifa), Bi. Magreth Ngomuo (Katibu Baraza) na Naibu Katibu Baraza Bw.
Tale Ndonje ni miongoni mwa viongozi ambao walifanikisha na kuhudhuria
Mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Maj. Gen. Projest Rwegasira akiwasili katika Chuo Cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA). |
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar akiwasili katika Chuo cha Uhamiaji Cha Kikanda (TRITA) kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano. |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akiwaongoza Makamishna wengine kumpokea Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi |
Wajumbe wakiwasili kwenye ukumbi wa mkutano |
Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji TRITA Commandant Maurice Kitinusa akiwakaribisha wajumbe |
Viongozi wa Baraza wakiwaongoza wajumbe kuimba wimbo wa Watumishi 'Solidarity forever' |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni