Idara ya Uhamiaji imepokea ujumbe wa Maafisa kumi na tisa (19) toka nchini Ivory Coast na Niger. Maafisa hao ambao ni viongozi waandamizi wa Serikali, Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM), Mashirika ya Kimataifa ya Kikanda ya AU, UEMOA na ECOWAS walifanya ziara ili kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi baina ya mataifa hayo ya Afrika Magharibi na Tanzania.
Mwenyeji wao Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Kamishna Hannelore Manyanga alipokea ujumbe huo katika Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya kusalimiana na kuingia ukumbi wa mikutano, wajumbe hao walipata maelezo mbalimbali ya Huduma zinazotolewa na Idara ya Uhamiaji.
Pia wajumbe hao walipata fursa ya kujifunza kuhusu taratibu za Uingiaji na Utokaji nchini, mifumo ya utambuzi na taarifa za wasafiri pamoja na masuala ya udhibiti na usimamizi wa mipaka.
Kiongozi wa ujumbe huo Bwana Ouba Ibrahim kutoka nchini Niger alimshukuru Kaimu Kamishna Jenerali kwa mapokezi mazuri na mkutano uliokuwa na lengo la kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi kati ya Uhamiaji Tanzania na idara za uhamiaji, polisi na forodha za nchi za Niger na Ivory Coast.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni