Kamishina Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna P. Makakala leo tarehe 21
Novemba 2017 amefanya zaiara ya kikazi na kukagua Ofisi na Vituo vya Uhamiaji
Mbalimbali Mkaoni Mara. Ofisi alizotembelea ni Shirati na Vituo vya
Mipakani wa Sirari (Mpaka wa Tanzania na Kenya) na Shirati katika Ziwa
Victoria, mpaka ambao unaunganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.
"Mkoa wa Mara umebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi ikiwemo
ziwa Victoria ambalo limekuwa ni kivutio kwa wahamiaji haramu kutoka nchi
jirani kuja na kufanya shughuli za uvuvi bila kufuata Sheria za nchi. Ni jukumu
la kila Mwananchi kuwa mlinzi wa rasilimali za Taifa na kuhakikisha kuwa
zinatumika kwa manufaa ya raia wa Tanzania na sio kwa wageni hususani wahamiaji
haramu" alisema Kamishna Jenerali.
Katika ziara
hiyo wilayani Rorya, Kamishna Jenerali aliyefuatana na Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi Mheshimiwa Hamad Masauni na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Adam
Malima walitembelea kituo cha uhamiaji Shirati na kukagua mpaka wa
Tanzania na Uganda katika ziwa Victoria. Pia alipata fursa ya kuongea na
wananchi katika kijiji cha Nyang'ombe kilichopo mwambao mwa ziwa Victoria
katika Wilaya ya Rorya na kuwaasa kushirikiana na Idara yake katika suala zima
la ulinzi wa mpaka huo na kuwasisitiza kutowahifadhi wahamu haramu.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akifafanua jambo kwa wananchi katka mpaka wa Sirari |
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Adam Malima akiwahutubia wanachi katika mpaka wa Sirari |
Kutoka kuusho, Mkuu wa Mkoa Mara, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji wakikagua mpaka wa majini baina ya Tanzania na Kenya katika ziwa Victoria. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni