Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

13 Agosti 2018

UHAMIAJI YAZINDUA HUDUMA YA PASIPOTI MPYA YA KIELEKTRONIKI JIJINI MWANZA.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela amezindua huduma mpya ya Pasipoti za Kielektroniki katika Jiji la Mwanza, hafla iliyofanyika katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoani Mwanza.

Mhe. Mongela amewataka Watanzania kuzitunza pasipoti zao kwa uangalifu na kuzitumia katika njia halali kwavile Pasipoti ni Utambulisho wa Utaifa wa mtu anaposafiri nje ya nchi.
Aidha, Afisa Uhamiaji wa Mkoa Mwanza, Kamishna Msaidizi Paul Eranga alieleza kuwa hadi sasa takribani Mikoa 21 imekwisha fikiwa na huduma tangu kuzinduliwa kwake Januari 23, 2018.

"Tunatarajia mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu, Idara itakuwa imekalimilisha kufunga Mifumo ya utoaji wa Pasipoti hizi Mpya za Kielektroniki kwa nchi nzima. Pia tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Mgufuli azindue Mfumo wa Uhamiaji Mtando hadi sasa Jumla ya Wanzania 30,941 wamepatiwa Pasipoti hizi mpya za Kielektroniki." Aliongeza Naibu Kamishna Eranga.





Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  Mhe. John Mongela akisaini kukiri kupokea Pasipoti mpya ya Kielektroniki mbele ya Mwenyeji wake Afisa Uhamiaji Mkoa Mwanza, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Paul Eranga.

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa Mwanza, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Joseph Mtenga  (kulia) akiwa pamoja na baadhi ya Maafisa Uhamiaji wa Mwanza wakifuatilia jambo katika hafla ya uzinduzi wa pasipoti mpya ya kielektroniki

Afisa Uhamiaji Mkoa Mwanza, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Paul Eranga akitoa taarifa ya huduma za Uhamiaji katika hafla ya Uzinduzi wa Uhamiaji Mtandao na Pasipoti Mpya za Kielektroniki Jijini Mwanza.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni