Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Injinia Evarist Ndikilo leo tarehe 24 Agosti 2018 amezindua Huduma ya Pasipoti za Kielektroniki katika Mkoa wake mjini Kibaha kwenye Ofisi za Uhamiaji mkoa wa Pwani.
Katika Uzinduzi huo, Mheshimiwa Ndikilo amewaka wananchi wanaopatiwa pasipoti hizo kuzitunza na kuzitumia kwa matumizi sahihi.
"
Unakuta mtu yupo humu nchini wala havuki mipaka lakini anatembea na pasipoti, hio si sahihi, tembea na kitambulisho cha Taifa na si pasipoti. Hii ni kwa ajili ya kuvuka mipaka ya nchi na si vinginevyo" alisisitiza Mkuu wa Mkoa.
|
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Placid Mazengo akiongea na wananchi wakati wa Uzinduzi huo |
|
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Injinia Evarist Ndikilo akiongea na wananchi wa mkoa wa Pwani wakati wa Uzinduzi wa Pasipoti za kielektroniki katika mkoa huo. |
|
Mkuu wa Mkoa Mhe. Ndikilo akimkabidhi pasipoti yake mmoja wa wananchi wa mkoa wa Pwani |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni