TAARIFA KWA UMMA:
UFAFANUZI
JUU YA “UZUSHI” UNAOENEA KWENYE TOVUTI NA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU IDARA YA
UHAMIAJI KUTANGAZA NAFASI ZA KAZI.
Katika
siku za hivi karibuni, kumekuwepo na uvumi unaoenezwa kupitia baadhi ya tovuti
na mitandao ya kijamii kuhusu kutangazwa kwa nafasi za ajira na Idara ya
Uhamiaji kwa ngazi ya Mkaguzi Msaidizi, Koplo na Konstebo. Tunaamini uvumi huo unaenezwa na watu au kikundi cha watu kwa nia ya
kujipatia maslahi yao binafsi au kwa malengo wanayoyafahamu wao.
Kufuatia
kuwepo kwa taarifa hizo, Idara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
- Idara
ya Uhamiaji haijatangaza nafasi
zozote za ajira katika kipindi cha hivi karibuni, hivyo tunawaomba
wananchi wasirubuniwe au kushawishiwa na mtu yoyote kutoa kitu chochote
ili waweze kusaidiwa kupata kazi Idara ya Uhamiaji.
- Taarifa
za kutangazwa nafasi za kazi zilizotolewa kupitia blogu husika na Mitandao
ya kijamii si za kweli, bali ni
uzushi uliofanywa na watu au kikundi cha watu kwa malengo wanayoyajua wao.
- Idara ya Uhamiaji, kama Taasisi ya
Serikali hutangaza nafasi za ajira
kwa uwazi kupitia Magazeti, Televisheni na Tovuti yake ambayo ni
‘www.immigration.go.tz’
- Idara inalaani na kukemea vikali
watu au kikundi cha watu kinachotoa taarifa za upotoshaji kuhusu Idara
kutangaza nafasi za kazi kama ambavyo imeripotiwa kwenye baadhi ya tovuti
na mitandao ya kijamii.
Imetolewa
na;
KITENGO CHA UHUSIANO,
MAKAO MAKUU, DAR ES SALAAM.
TAREHE: 01 FEBRUARI, 2018
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni