Mkuu wa Utawala na Fedha kutoka Idara ya Uhamiaji Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACI) Gharib Saleh Suleiman, ameipongeza idara ya Uhamiaji Tanzania kwa kuendelea kutoa huduma bora za kiuhamiaji.
Ameyasema hayo mapema leo hii alipofanya ziara ya kutembelea Maonesho ya saba saba na kufurahishwa na namna idara ilivyojipanga kuwahudumia raia wa Tanzania na wageni mbalimbali waliotembelea banda hilo.
Baadhi ya Huduma zinaotolewa katika maonesho hayo ni pamoja na Elimu kwa ujumla juu ya huduma za Kiuhamiaji, ikiwemo Pasipoti, Uraia, visa, vibali vya Ukaazi, Udhibiti wa Mipaka nk.
Aidha SACI Suleiman alipata pia wasaa wa kutembelea mabanda mengine ya Maonesho yakiwemo ya JKT, Wizara ya Uvuvi, Mabanda ya Wajasiriamali kutoka, Zanzibar na Banda la Karume.
Maonesho haya ya 44 ya Biashara ya (DIFT) 2020 yalifunguliwa rasmi hapo jana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Katika Viwanja vya Saba Saba Vilivyopo Wilaya ya Temeke Jijini Dar es saalam.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Mkuu wa Utawala na Fedha kutoka Idara ya Uhamiaji Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACI) Gharib Saleh Suleiman alipotembelea banda la Uhamiaji katika Maonesho ya Saba saba |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni