Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

11 Julai 2020

CGI Dkt. Anna Makakala Afanya Ukaguzi wa Kiwanja Cha Ofisi ya Uhamiaji (W) Pangani na Kukagua Bandari ya Kipumbwi

Pangani, Tanga
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala ameendelea na ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Tanga, ambapo mapema wiki hii amewasili katika Wilaya ya Pangani na kufanya ukaguzi wa Kiwanja kipya kinachotarajiwa kujengwa Ofisi mpya ya Uhamiaji katika wilaya ya Pangani.

Hali hiyo imekuja baada ya Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Pangani kutumia majengo ya Halmashauri ya wilaya ambayo hayatoshelezi mahitaji ya utoaji wa huduma za kiuhamiaji kwa sasa.

CGI Dkt. Makakala ameupongeza uongozi wa ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Pangani na Mkoa kwa ujumla kwa kuwa na dira nzuri ya kuhakikisha wanamiliki viwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi mpya za Uhamiaji.

Aidha ametoa rai kwa Maofisa Uhamiaji Wilaya na Mikoa yote nchini kuwa wabunifu na kuhakikisha wanapata viwanja bora vitakavyosaidia katika ujenzi wa ofisi mpya pale ambapo zitaingizwa katika bajeti kwa ajili ya utekelezaji na lengo la Uhamiaji kwa ujumla ni kuhakikisha Wilaya na Mikoa yote nchini inamiliki Ofisi zake.

Wakati huohuo, Kamishna Jenerali Dkt. Makakala amefanya ukaguzi wa Bandari iliyoanzishwa hivi karibuni katika Wilaya ya Pangani maarufu kama Bandari ya Kipumbwi ambapo kuna shughuli nyingi za Kiuchumi kama vile uvuvi na usafiri wa kwenda Zanzibar ambapo shughuli za kiuhamiaji pia hufanyika.

Akitoa taarifa ya utendaji kazi Afisa Uhamiaji Wilaya ya Pangani Mrakibu Jenesta Ndeyetabula amesema Ofisi ya Uhamiaji wilayani hapo imeendelea kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na maelekezo mbalimbali yanayotolewa kutoka ngazi za juu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Pangani imeendelea kutoa huduma mbalimbali kama vile utoaji wa hati za dharula kwa njia ya kielekroniki, kupokea maombi ya uraia, kufanya uhakiki wa uraia na kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma za kiuhamiaji na namna ya kukabiliana na wahamiaji haramu.

Aidha Doria na ukaguzi wa mara kwa mara umeendelea kufanywa katika maeneo mbalimbali kama vile kizuizi cha feri, Bandarini, Hoteli za kitalii na nyumba za kulala wageni  ili kubaini wageni walioingia kwa kufuata taratibu na wasiofuata taratibu za kiuhamiaji kwa lengo la kuimarisha ulinzi na Usalama wa Taifa.

Ziara ya Kikazi ya Kamishna Jenerakli wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala Mkoani Tanga iliendelea tena katika Wilaya za Muheza, Korogwe, Lushoto na Handeni.

HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akisalimiana na OCD wa Wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake ya kikazi Walayani humo, mapema wiki hii 
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Pangani Bw. Issaya Mbenje wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya PanganiKamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akisaini Kitabu cha Wageni Katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Pangani na Kufanya Kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo 
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Pangani Akitoa Taarifa fupi ya hali ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Pangani Kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga Mrakibu Mwandamizi Mbaraka Batenga akitoa Utambulisho


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiwa katika Picha ya Pamoja na OCD wa Wilaya ya Pangani wa Kwanza Kushoto, Afisa Uhamiaji Wilaya ya Pangani na Staff officer wa Uhamiaji Mkoa wa Tanga. 

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akielekea katika ofisi za sasa za Uamiaji (W) Pangani (katikati) ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga  SSI Batenga na (Kulia pichani) ni Konstebo wa Uhamiaji Faustine Mayenga wa kituo cha Uhamiaji Wilayani hapo 


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akisalimia Wananchi mbalimbali aliokutana nao wakati wa ziara yake Wilayani Pangani
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akioneshwa mpaka wa Kiwanja Kitakapojengwa Ofisi Mpya ya Uhamiaji Wilaya ya Pangani
Konstebo wa Uhamiaji Faustine Mayenga akisimama katika Mpaka Mwingine kuonesha Kiwanja cha Uhamiaji Wilaya ya Pangani Tayari kwa Taratibu za Mipango ya Kuanza Ujenzi wa Ofisi hiyo mpya ya Wilaya 
Muonekano wa Kiwanja Kitakapojengwa Ofisi Mpya za Uhamiaji Wilaya ya Pangani
Ukaguzi wa Kiwanja Ukiendelea

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akielekea kuvuka kivuko cha MV Tanga kuendelea na  ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Pangani
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akisalimia Wananchi waliokuwa katika eneo la kivuko wakati  akiendelea na  ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Pangani

Ndani ya Kivuko cha MV TangaKamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akivuka katika kivuko cha MV Tanga kuendelea na  ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Pangani


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiongozwa na Mtendaji wa Kijiji (Mwenye Shati Jeupe) kukagua Bandari iliyoanzishwa hivi karibuni ya Kipumbwi iliyopo  Wilayani Pangani


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akipata maelezo ya awali kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipumbwi (Mwenye Tisheti Nyekundu) wakati akikagua Bandari iliyoanzishwa hivi karibuni ya Kipumbwi iliyopo  Wilayani Pangani


Ukaguzi UkiendeleaBaadhi ya Wananchi wanaojishughulisha na uvuvi katika Kijiji cha Kipumbwe Wilayani PanganiKamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kipumbwi (Hawapo Pichani) wakati wa ziara yake ya  kukagua Bandari iliyoanzishwa hivi karibuni ya Kipumbwi iliyopo  Wilayani Pangani


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiongea na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Wilayani Pangani baada ya kumaliza ziara ya kikazi Wilayani humo

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akimaliza ziara yake ya Kikazi Wilayani Pangani na sasa Kuelekea Wilaya ya Muheza (Picha Zote na Kitengo cha Habari na Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni