Handeni, Tanga
Mkuu Mpya wa Wilaya ya Handeni Mhe. Toba Anason Nguvila ikiwa ni siku yake ya kwanza kuripoti na kuanza kazi katika ofisi yake kwa nafasi ya Ukuu wa Wilaya, amepata Baraka za kutembelewa na Kiongozi wa ngazi za juu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala wakati wa ziara yake ya Kikazi aliyoifanya hivi karibuni Mkoani Tanga ambapo alitembelea Karibu Wilaya zote, na kukagua vituo vyote vya Uhamiaji na Mipaka ya nchi iliyopo katika Mkoa huo, ambapo hali ya Ulinzi na Usalama ni shwari.
Dkt. Makakala amempongeza Mhe. Nguvila kwa kuteuliwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kumuwakilisha katika wilaya hiyo na hivyo amemtakia kila la heri na mafanikio mema katika kutekeleza majukumu hayo aliyopangiwa kwa manufaa ya wana Handeni na Taifa kwa ujumla.
Mhe. Nguvila amechukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Handeni Mhe. Godwin Gondwe ambaye hivi karibuni amepangiwa kituo kingine cha Kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake Mhe. Nguvila alimshukuru Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Makakala kwa uongozi wake Imara na uliotukuka katika kuingoza vyema Idara ya Uhamiaji ambapo huduma za kiuhamiaji zimeboreshwa na zinapatika kwa viwango vya kimataifa na ubora wa hali ya juu sana.
“Tunatambua kazi yako nzuri unayoifanya katika Idara ya Uhamiaji, na hasa kwenye Pasipoti sasa hivi tunabofya kielekronikia tofauti na zamani tulikuwa kwenye vitabu, lakini pia hongera kwa kazi nzuri inayofanwa ya kutambua walowezi” alisema Mhe. Nguvila.
Kwa Mujibu wa Mkuu wa Wilaya Handeni Mhe. Nguvila, Wilaya hiyo ni Moja kati ya Wilaya Kubwa zilizopo katika Mkoa wa Tanga ambapo ina Halmashauri 02, Halmashauri ya Mji Handeni na Halmashauri ya Wilaya Handeni Vijijini, Tarafa 07, Kata 23 na Mitaa 60 ya Halmashauri ya Mji Handeni, sanjari na Idadi ya watu inayokadiriwa kuwa zaidi ya laki nne (400, 000).
HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akipokea taarifa ya hali ya ulinzi na usalama kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Handeni Mhe. Toba Nguvila ( Hayupo Pichani) |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiwa katika Picha ya Pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Handeni |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiagana na Afisa Usalama (W) Handeni |
Pichani, Baadhi ya Maofisa na Askari wa Uhamiaji na Magereza (W) Handeni wakijiaandaa kumpokea Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala katika Ofisi za Uhamiaji Wilayani hapo. |
Baadhi ya Maofisa na Askari wa Uhamiaji na Magereza (W) wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala katika Ofisi za Uhamiaji Wilaya ya Handeni . |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni