Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

20 Julai 2020

Habari Picha na Matukio ziara ya CGI Dkt. Makakala Wilayani Lushoto

Lushoto, Tanga
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala aliendelea na ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Lushoto ambapo alifanya kikao na kupokea taarifa ya hali ya ulinzi na usalama kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa ya Wilaya ya Lushoto  Mhe. January Lugangika na baadae kutembelea Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Lushoto na kuongea na Maofisa na askari wa Uhamiaji wa Wilaya hiyo

Ziara yake iliendelea Wilayani Korogwe Mkoani Tanga na kumalizia Katika Wilaya ya Handeni.


HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akipokelewa na Mkuu wa Wilaya Lushoto Mhe. January Lugangika Wakati wa ziara yake ya kikazi hivi karibuni Mkoani Tanga


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akisaini kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Lushoto Mkoani Tanga



Mkuu wa Wilaya Lushoto Mhe. January Lugangika


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiangalia gari inayotumiwa na Maofisa Uhamiaji Wilaya ya Lushoto(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni