Dodoma,
Tanzania
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna
Makakala amelishukuru Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) Tanzania kwa
kuchangia vifaa mbali mbali vitakavyosaidia katika kuimarisha usimamizi na
Udhibiti wa Mipaka nchini.
Ameyasema hayo jana Jijini Dodoma katika Ofisi za
Makao Makuu ya Uhamiaji Tanzania baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kutoka kwa
Kiongozi wa shirika hilo hapa nchini (IOM-Tanzania Chief of Mission) Dr. Qasim
Sufi.
Vifaa vilivyotolewa ni Pikipiki 5 aina ya
Honda XL125, Darubini 6 (6 pairs of High
Magnification Infrared Binoculars), Mifuko 8 ya Kambi (8 Camping Tents), Boksi
18 za vifaa vya kutolea Msaada wa huduma ya kwanza na Tochi 18.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni