Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

07 Septemba 2020

Mafunzo ya Uhamiaji kwa Wadau (TRITA) Yaendeleza Dira ya Idara ya Uhamiaji na Kukuza Maendeleo ya Kiuchumi

Moshi, Kilimanjaro

Mafunzo ya Usimamizi wa Masuala ya Kiuhamiaji yameanzishwa kwa lengo la kuendeleza dira ya Idara ya Uhamiaji ili kuwezesha na kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu kupitia utekelezaji wa sheria na kanuni zilizopo ili kulinda usalama wa Taifa na kukuza maendeleo ya kiuchumi.

Akihitimisha mafunzo hayo ya usimamizi wa masuala ya kiuhamiaji kwa wadau walioshiriki  kutoka katika taasisi na mashirika mbali mbali ya umma na binafsi yaliyofanyika katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Abdallah Towo ameeleza namna mafunzo hayo yanavyochangia katika maendeleo ya Taifa.

DCI Towo amebainisha kwamba mafunzo hayo yanasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya idara na taasisi za umma na binafsi kwa lengo la kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji biashara nchini hasa kwa kuzingatia dhana ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya Viwanda.

Hata hivyo mafunzo hayo huwasaidia pia sekta binafsi kufahamu jinsi wanavyoweza kushiriki katika usimamizi wa masuala ya Uhamiaji nchini sanajari na watendaji wa taasisi za umma kufahamu sheria, Kanuni, taratibu na mingozo ya mara kwa mara inayotolewa na idara kuhusu utoaji wa nyaraka zake mbalimbali.

“Mafunzo haya husaidia pia kuondoa utaratibu wa kutumia vishoka  ( Middlemen) katika upatikanaji wa huduma mbalimbali za kiuhamiaji na hatimae kusaidia kutambuliwa rasmi katika kanzi data ya Idara ya Uhamiaji ili kuwawezesha kupata huduma bila vikwazo vyovyote” alisema DCI Towo

Kwa upande wao washiriki wamemshukuru Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna Makakala kwa kupata fursa hiyo ya kushiriki mafunzo pia wameupongeza uongozi wa chuo pamoja na wakufunzi kwa kuwapa shule ya kutosha kuhusu masuala ya Kiuhamiaji na Wameahidi kwenda kuwa mabalozi wazuri wa Masuala ya Kiuhamiaji na kuelimisha  wengine kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae na hatimae kukuza maendeleo ya kiuchumi.

Chuo Kinaendesha mafunzo ya usimamizi wa masuala ya kiuhamiaji kwa wadau wa masuala ya Kiuhamiaji nchini, na hushirikisha maafisa watendaji na wamiliki wa biashara mbalimbali zinazohudumia wageni ama kuajiri wageni au kufanya biashara na wageni.

Hali hii imekuja  kutokana na mabadiliko yanayotokana na sekta ya uhamiaji chuo kimetanua wigo na sasa kinatoa mafunzo ya usimamizi wa masuala ya Uhamiaji kwa taasisi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mkakati mahsusi wa Idara ya uhamiaji kuwashirikisha wadau wengine katika usimamizi wa masuala ya Uhamiaji nchini.

Mafunzo haya yalifunguliwa rasmi tarehe 01 Oktoba 2019, mpaka sasa jumla ya awamu saba za mafunzo zimeshafanyika huku zikishirikisha jumla ya taasisi 146 na washiriki 180, aidha mafunzo haya hufanyika kila mwezi ambapo mwezi huu Septemba 2020 jumla ya wahitimu 19 wamehitimu mafunzo yao ambayo yalishirikisha pia Benki ya NBC Moshi na mafunzo yajayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 05 Oktoba 2020.

Chuo cha Uhamiaji Cha Kikanda (The Tanzania Regional Immigration Training Academy (TRITA) Kilianzishwa mwaka 2007 na kufunguliwa rasmi tarehe 12 Disemba 2008 baada ya kusajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa lengo la kutoa mafunzo ya kuwajengea na kukuza uwezo wa kiutendaji wa watumishi wa Idara ya Uhamiaji na wadau wengine wa masuala ya kiuhamiaji kitaifa na kimataifa pamoja na kutoa mafunzo kwa maafisa na Askari  wanaotarajiwa kuajiriwa na uhamiaji.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Pichani Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji (TRITA) DCI Abdallah Towo (Katikati Waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Mafunzo ya Masuala ya Kiuhamiaji


Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji (TRITA) DCI Abdallah Towo akiongea na Washiriki, Maofisa na Askari wa Uhamiaji (Hawapo Pichani) wakati wa Kufunga Mafunzo

Mmoja wa Washiriki Vivienne Mtei akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Chuo TRITA DCI Towo


Meneja wa Benki ya NBC Moshi Bw. Lazaro Mollel akitoa neno kwa washiriki
Mshiriki wa Mafunzo Bw. Wilfred Megiroo akipata picha ya Ukumbusho na Meneja wa Benki ya NBC Moshi Bw. Lazaro Mollel




Washiriki wa Mafunzo



Mmoja wa Washiriki Bw. Cletus Majani akipokea cheti








Mshiriki Monica Caspary nae akipata cheti cha ushiriki


Cristabell Isaac akipata Cheti cha Ushiriki wa Mafunzo





Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji (TRITA) DCI Abdallah Towo akiongea na Washiriki wa Mafunzo wakati wa Hitimisho




Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji (TRITA) DCI Abdallah Towo akibadilishana mawazo na Meneja wa Benki ya NBC Moshi Bw. Lazaro Mollel baada ya kuhitimisha mafunzo



Picha ya Pamoja

(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni