Dodoma, Tanzania
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala mapema leo hii amekagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo Jipya la Ofisi za Uhamiaji Makao Makuu Dodoma.
Akiwa Katika Ukaguzi huo amejiridhisha na Ubora wa Ujenzi lakini ameitaka kampuni ya Ujenzi ya SUMAJKT Inayotekeleza Mradi huo Kuongeza Kasi ya Ujenzi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya Kukamilisha kazi hiyo ya Ujenzi kwa Viwango vya Ubora wa Hali ya Juu na kwa wakati muafaka uliopangwa.
Ujenzi huo ni matokeo chanya ya Serikali ya awamu ya tano Kuhamishia Makao Makuu ya Nchi rasmi Jijini Dodoma Chini ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha Mhe. Rais Dkt. Magufuli wakati wa Uzinduzi wa Mfumo wa Uhamiaji Mtandao (e-Immigration) uliofanyika Jijini Dar e salaam Tarehe 31 Januari 2018 alitoa Tsh.Bilioni 10 kwa ajili ya Kuanza Ujenzi huo wa Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji Tanzania ambao utakamilika hivi karibuni ukiwa na ghorofa nane.
HABARI PICHA NA MATUKIO
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala Akitoa Maelekezo kwa Wataalamu wa Ujenzi wa Kampuni ya SUMAJKT Mapema leo hii Jijini Dodoma Ili kuongeza Kasi ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji Tanzania |
|
Mtaalamu wa Ujenzi Kutoka Kampuni ya Ujenzi ya SUMAJKT Akitoa maelezo ya awali ya maendeleo ya Ujenzi kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala akitoa maelekezo |
|
Ujenzi Unaendelea |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala akitoa maelekezo |
|
Ujenzi Unaendelea |
|
Mafundi Wakiendelea na Kazi |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala akiendelea na Ukaguzi |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala akiendelea na Ukaguzi wa Ujenzi |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala akishuka katika Ngazi mara baada ya Kumaliza Ukaguzi na Kutoa Maelekezo ya Kuhakikisha Kasi inaongezeka ya Ujenzi |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala akisisitiza jambo kwa Wataalamu wa Ujenzi wa SUMAJKT |
|
Ujenzi ukiendelea |
|
Mtaalamu wa Ujenzi kutoka SUMAJKT akimhakikishia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala Kuongeza Kasi ya Ujenzi |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala Akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kumaliza Ukaguzi wa Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi Mpya za Uhamiaji Makao Makuu Dodoma (Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Nzuri iyo
JibuFutaNimefurahishwa sana na hii habari kwa njia hii ya picha nzuri za mradi huo kazi nzuri
JibuFuta