Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

02 Septemba 2020

Bonanza la Michezo la Vyombo vya Ulinzi na Usalama lafana sana

 Dar es salaam

Umoja, Utulivu na mshikamano tunaojivunia Watanzania vimetokana na utamaduni tuliojijengea tangu enzi ya utawala wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Katika kudumisha mshikamano na ushirikiano Vyombo vya ulinzi na usalama nchini vimeshirikiana katika bonanza la michezo mbalimbali ambalo hufanyika kila mwisho wa mwezi kwa lengo la kujenga  na kudumisha uhusiano, ushirikiano, umoja na Mshikamano baina ya vyombo hivyo.

Bonanza hilo limefanyika jijini Dar es salaam Wilaya ya Temeke katika viwanja vya Jeshi Mgulani Twalipo huku vikihusisha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ,Polisi, Magereza, Uhamiaji, na Zimamoto.

Maofisa na askari wa Uhamiaji kwa wakati tofauti wamezungumzia faida wanayopata ya kufanya mazoezi kwa pamoja kwani yanajenga utimamu wa afya ya mwili na kuleta utimamu wa kiakili kijamii na kutokuwepo kwa maradhi ambayo ni nguzo na  rasilimali muhimu ya kuchangia maendeleo ya mtu binafsi, familia na nchi kwa ujumla katika kuleta maisha bora na kupunguza umaskini.

 HABARI PICHA NA MATUKIO




Mbio za Asubuhi







Mazoezi ya Viungo






































(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni