Kigoma, Tanzania
Kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala ametoa maagizo
hayo Mkoani Kigoma akiwa katika ziara ya Kikazi ya Kukagua mipaka ya nchi na
kukagua utendaji kazi wa Maafisa na Askari wa Uhamiaji ambapo amewataka Maafisa
Uhamiaji Mikoa kote nchini kuhakikisha wanatekeleza agizo la kuwa na Maafisa Uhamiaji Kata kwa kila kata kote
nchini ili kusogeza huduma karibu kwa
wananchi.
“Niwatake Maafisa Uhamiaji kote nchini kuhakikisha mnatekeleza magizo
haya na pia kutoa mawasiliano kwa wanachi ili waweze kufikisha shida zao na pia
kusaidia kutoa taarifa za wahamiaji haramu katika maeneo yao ili tukomeshe
kabisa suala la wahamiaji haramu” alisema
Aidha amewataka pia kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya
Kiuhamiaji kwa kutumia njia mbalimbali
zikiwemo za televisheni redio, Magazeti Mikutano na warsha mbalimbali.
Hata hivyo CGI Dkt. Anna Makakala ameelekeza pia Maafisa na askari
kuendelea kufanya kazi kwa, utii uhodari, uzalendo, Uwajibikaji na kwa weledi
wa hali ya juu sanjari na kuwa na upendo, mshikamano na ushirikiano na vyombo
vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha ulinzi na Usalama Mipakani
Unaimarishwa Ipasavyo kwa kufanya doria na misako ya mara kwa mara hasa wakati
huu wa Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani.
Aidha ametoa rai kwa wananchi wote kushirikiana na vyombo vya ulinzi na Usalama katika Kuilinda mipaka ya nchi sanjari na kuwahakikishia Wananchi wa Kigoma katika kuongeza kasi ya Kuwahudumia ili waweze Kupata vitambulisho vya Taifa kwa wakati hasa kwa Kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA.
Akitoa taarifa ya Utendaji kazi ya Mkoa wa Kigoma, Afisa Uhamiaji Mkoa Naibu Kamishna wa
Uhamiaji (DCI) Remigius Pesambili amesema katika kupunguza wimbi la uhamiaji
haramu Mkoani Kigoma Mkoa umekuwa ukifanya Misako doria na operesheni katika
maeneo mbalimbali ambapo kwa kipindi cha mwezi Julai 2019 mpaka Agosti 2020
wamekamatwa wahamiaji haramu 5576 na kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa
sheria ikiwepo kufikishwa Mahakamani na wengine kurudishwa nchini kwao.
Akiongelea Mikakati ya Kudhibiti wahamiaji haramu DCI Pesambili amesema
kwamba Mkoa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kigoma inatekeleza mkakati wa kutokomeza
kabisa wimbi la wahamiaji haramu kwa kuendelea na misako na doria, Kimarisha
Vizuizi vya barabarani katika maeneo yote ya kimkakati, kuimarisha mpango wa
utoaji elimu ya uraia na athari
zitokanzo na uingiaji wa wahamiaji haramu
sanjari na kuanzisha mpango wa kugawa kata
kwa kila Afisa Uhamiaji ili kusogeza huduma karibu na wananchi na
kusaidia kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu kuanzia ngazi ya chini mpaka juu.
Katika kuhakikisha shughuli za Uhamiaji katiaka Mkoa wa Kigoma zinatekelezwa
kwa ufanisi na kudhibiti uhamiaji
haramu Mkoa umeomba kupatiwa mafunzo ya
mara kwa mara ambayo hasa yanahusiana na msuala ya Intelejensia Katika Udhibiti
wa mipaka.
Katika ziara yake Kamishna Jenerali Wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala
ametembelea karibu wilaya zote za Mkoa wa Kigoma ikiwemo Wilaya ya Kakonko,
Kibondo, Kasulu Buhigwe, Kigoma Mjini na vituo vya Uhamiaji vya kutoka na
kuingia nchini vikiwemo vituo vya Mabamba , Manyovu, Kibirizi, Ujiji, Bandari
ya Kigoma na Kibirizi.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akiwa katika Picha ya pamoja na Askarina watumishi wa Uhamiaji katika Ofisi ya Mkoa Kigoma |
Kamishna Jenerali wa uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiwa katika Picha ya pamoja na Maofisa na Askari wa Uhamiaji Wilaya ya Kasulu |
Afisa Uhamiaji Mkoa Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Remigius Pesambili Akitoa taarifa ya Utendaji kazi ya Mkoa |
Kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Askari wa Uhamiaji Wilaya ya Kasulu |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni