Kigoma, Tanzania
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna Makakala akiwa na Wakuu wenzake wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mapema leo hii Wamehudhuria Ziara rasmi ya Rais wa Burundi Mhe. Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye iliyoifanyika Mkoani Kigoma huku ikiongozwa na Mwenyeji wake Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye aliwasili Mjini Kigoma majira ya Asubuhi na kupokelewa na mwenyeji wake Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyeambatana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi, Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mfunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Isack Kamwelwe na Viongozi wengine waandamizi wa kiserikali sanjari na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake walizungumza na watanzania katika uwanja wa Lake Tanganyika uliopo mjini Kigoma Kabla ya kuzindua Jengo la Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma na baadae walifanya mazungumzo rasmi Katika Ikulu ndogo ya Kigoma
Ziara hii ni ziara rasmi na ya kwanza kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye kutembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu kuingia kwake madarakani .
HABARI PICHA NA MATUKIO
|
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna Makakala baada a Kumaliza Ziara yake rasmi nchini Tanzania |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye wakati wa Kupokea saalamu ya Heshima kutoka katika Gwaride Maalumu lililoandaliwa |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Wakuu wa Vyombo na Ulinzi na Usalama |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Wakuu wa Vyombo vya ulinzi na Usalama |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akimuaga Rais wa Burundi Mhe. Meja Jenerali Evariste Ndayishimie Kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna Makakala |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna Makakala akiteta jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa |
|
Pichani ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna Makakala akiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Suleiman Mzee (Katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma (CP) Thobias Andengenye |
|
Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma iliyozinduliwa na Rais wa Tanzania na Burundi
|
|
Uzinduzi rasmi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma
|
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango |
|
Kikundi cha Gwaride Maalumu la Heshima kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania |
|
Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo alisalimiana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna Makakala wakati wa Ziara Rasmi ya Rais wa Burundi iliyofanyika Mkoani Kigoma Mapema Leo Hii (Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni