Moshi, Kilimanjaro
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Naibu Kamishna wa Uhamiaji Abdallah Ramadhan Towo amefungua mafunzo ya usimamizi wa masuala ya kiuhamiaji kwa taasisi na sekta binafsi yanayofanyika chuoni hapo kwa muda wa siku tano, Mkoani Kilimanjaro
DCI Towo amesema, mafunzo hayo yaliandaliwa mahsusi ili Kuziwezesha sekta binafsi na tasisi nyingine za kiserikali kufahamu kwa kinaga ubaga masuala ya kiuhamiaji na Idara ya Kazi, ili kuimarisha uhusiano na kuboresha utoaji huduma kwa watanzania na wageni waishio na kufanya kazi nchini.
Vilevile ameleza kuwa, mafunzo hayo yamekuja kufuatia uelewa mdogo wa wadau mbalimbali kuhusu kanuni, sheria, na miongozo mbalimbali inayotolewa na huduma za kiuhamiaji na Idara ya Kazi, hivyo kupelekea kupoteza muda mwingi katika kupata huduma za kiuhamiaji jambo linalo pelekea kuongezeka kwa rushwa, kuwepo kwa hati bandia, na kuisababisha serikali kukosa mapato.
Kupitia mafunzo hayo, taasisi na sekta binafsi watapata kujifunza masuala muhimu yahusuyo vibali vya ukaazi, uraia, visa, udhibiti wa wageni na masuala mengine kadha wa kadha yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha, Naibu Kamishna amewaomba taasisi za sekta binafsi kujenga mshikamano na mahusiano mazuri na Idara ya Kazi na Uhamiaji katika utendaji wa kazi zao.
Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Benki ya NBC huku yakihudhuriwa pia na Kaimu Mkufunzi Mkuu wa Chuo, Mrakibu Ignitious Mgana Mwakilishi toka IOM/ACBC na Mkufunzi toka Idara ya Kazi.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Pichani (Katikati) ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Naibu Kamishna wa Uhamiaji Abdallah Ramadhan Towo akifungua Mafunzo |
Baadhi ya Washiriki wengine wakifuatilia kwa makini mafunzo katika chuo cha Uhamiaji (TRITA) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni