Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

10 Septemba 2020

CGI Dkt. Anna Makakala Afanya Ziara ya Kushtukiza JNIA Na Kufanya Ukaguzi wa Pasipoti kwa Abiria Waliowasili

Dar es salaam

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji  CGI Dkt. Anna Makakala amefanya ziara ya Kushitukiza katika Uwanja wa ndege wa Kimatifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA) Uliopo jijini Dar es salaam na kufanya ukaguzi wa Pasipoti kwa wageni na raia waliowasili uwanjani hapo kwa ndege ya Shirika la Ethiopia.

Akiongea na Waandishi wa Habari Uwanjani Hapo CGI Dkt. Makakala amesema amefika uwanjani hapo ikiwa ni moja ya ziara zake za kikazi ambapo hutembelea mipaka na vituo vya uhamiaji nchini kufanya ukaguzi wa mipaka na kukagua utendaji kazi wa Maafisa na Askari wa Uhamiaji katika maeneo yao ya kazi.

Uhamiaji  ni chombo cha ulinzi na usalama kinachofanya kazi kwa mujibu wa sheria ya uhamiaji sura ya 54 ya mwaka 2016 kikiwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi huku ikiwa na majukumu me   ngi ikiwemo ulinzi na udhibiti wa mipaka ili kuhakkisha nchi inakuwa salama muda wote.

Katika Udhibiti wa mipaka Idara ya Uhamiaji tunatumia sheria na wageni wote wanaoingia nchini ni lazima wafuate sheria kanuni na taratibu za Uhamiaji nan chi kwa ujumla.

“Sisi Tanzania kama mnavyoiona tuna mipaka mingi sana, tumezungukwa nan chi takribani 08 ambazo mipaka yake ni mikubwa na mipana, lakini tupo katika mipaka yote, tuna vituo vya kutolea huduma za kiuhamiaji zaidi ya 80, hivyo tunawataka wageni wote na raia wa Tanzania kutumia utaratibu wa kuingia na kutoka nchini kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma vilivyorasimishwa kwa mujibu w sheria na si vinginevyo” alisema CGI Dkt. Makakala.

CGI Dkt. Makakala amesisitiza kwamba mtu yeyote atakae vunja sheria, ni lamiza sheria ichukue mkondo wake kwani haita angalia  kwamba mgeni huyu au raia huyu ni kiongozi wa nyadhifa gani sheria ni msumeno inakata kote kote.

“Tupo kwenye kipindi cha uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani ni lazima tuhakikishe tunaumaliza uchaguzi wetu salama, lakini pia tumeongeza nguvu mipakani na kufanya doria na misako ya mara kwa mara ili kuilinda nchi yetu, nawaomba sana Watanzani tushirikiane katika kuilinda mipaka yetu kwani jukumu la ulinzi na usalama wa nchi yetu ni letu sote” Alisema.

HABARI PICHANA MATUKIO

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji  CGI Dkt. Anna Makakala Akimhoji Mmoja wa wageni aliyewasili nchini kwa ajili ya Utalii


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji CGI Dkt. Anna Makakala akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo Pichani)


Afisa wa Uhamiaji akikagua Pasipoti ya Mgeni aliyewasili nchini


Kamishna wa Pasipoti na Uraia Gerald Kihinga akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji  CGI Dkt. Anna Makakala anaefuatia ni Mfawidhi Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji (JNIA) DCI Albert Rwelamira 


Ndege iliyowasili na abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. JK Nyerere



(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni