Kamishna wa Utawala na Fedha Peter Chogero akimsalimia Mkurugenzi mkuu mstaafu wa Idara ya Uhamiaji Rafael Kubaga aliyestafu miaka miaka 30 iliyopita |
Mwenyekiti wa Uhamiaji SACCOS akimsalimia Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Uhamiaji Rafael Kubaga wakati walipomtembelea nyumbani kwake Keko jijini Dar es salaam |
Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha Peter Chogero, Makamishna
wa Uhamiaji Sheria na Viza Hanelore Manyanga na Salum Mwichumu, Mwenyekiti wa Saccos ya Uhamiaji Mrakibu Msaidizi Mdeme Charles, Leo tarehe 24 Disemba 2018 wamewatembelea wagonjwa ambao ni watumishi wa
idara ya Uhamiaji pamoja na wastaafu kuwajulia hali zao pamoja na kuwapatia zawadi
ya krismasi zilizotolewa na Uhamiaji SACCOS
“Kwa niaba ya Kamishna Jenerali na watumishi wote wa idara
ya Uhamiaji tumekuja kuwaona ndugu zetu kujua mnaendeleaje na afya zenu tumekuja kuwapatia zawadi za krismasi na mwaka
mpya kwa niaba ya afande Jenerali Anna Makakala ambaye ndio mlezi wa SACCOS kuonyesha
bado tuko na ninyi katika kipindi hiki cha ugonjwa”amesema Kamishna Chogero
Aidha Kamishna Chogero amesema Idara ya Uhamiaji ipo
pamoja na watumishi waliopo kazini na wastaafu ndio maana Uhamiaji SACCOS imewakumbuka
kwa kutoa zawadi ya sikuku ya krismasi ili wafurahie vizuri.
Kwa upande wa Kamishna Mstaafu Dowson Mongi amesema “Namshukuru
sana Kamishna Jenerali Anna Makakala kwa upendo anaotuonyesha kwa wastaafu na
wagonjwa inaonyesha jinsi gani anatuthamini sie wastaafu,mungu aendelee kuwapa
moyo wa upendo watumishi wote wa Idara ya uhamiaji”
Pamoja na ziara hiyo ya kuwatembelea wagonjwa Kamishna
Chogero na Kamishna Mwinchumu wamewatakia watumishi wote wa idara ya Uhamiaji heri
ya krismasi na mwaka mpya.
Aidha amewakumbusha wananchi kutoa taarifa ya Uhamiaji au
vyombo vya Dola pale wanapoona watu au makundi ya watu wanaohisiwa kuwa ni
wahamiaji haramu hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za Krismasi na mwisho wa Mwaka
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni