Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

28 Februari 2025

MAMIA WAJITOKEZA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MRAKIBU MWANDAMIZI WA UHAMIAJI (SSI) AMON MOGHA.

Na. A/Insp Amani Mbwaga, Dodoma.


Mamia ya Maafisa, Askari Watumishi wa Umma na Wananchi wamejitokeza leo tarehe 28 Februari 2025  Chidachi Jijini Dodoma kuaga Mwili wa Marehemu Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI)Amon Oscar Mogha aliyefariki  ghafla jioni ya tarehe 25 Februari 2025 njiani alipokuwa anatoka mazoezini Jijini Dodoma. 

Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Julieth Sagamiko, Kwa niaba ya Kamisha Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala aliwaongoza mamia ya Watu Jijini Dodoma wakiwemo Maafisa, Askari, Watumishi wa Umma na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Dodoma na Tanzania kwa jumla kuuwaga Mwili wa marehemu.

Akitoa salamu za rambi rambi DCI Sagamiko amesema Marehemu SSI Mogha amefariki katika kipindi ambacho Idara ya Uhamiaji bado ilikuwa inahitaji mchango wake kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza majukumu yake.