Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

29 Julai 2018

28 Julai 2018

ASKARI NA MAAFISA UHAMIAJI WAHITIMU MAFUNZO YA UPANDISHWAJI VYEO KATIKA SHULE YA POLISI MOSHI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu amefunga mafunzo ya upandishwaji vyeo kwa askari na maafisa uhamiaji yaliyofikia tamati siku ya tarehe 27 Julai 2018. Mafunzo hayo ya miezi mitatu yaliyofanyika Shule ya Polisi Moshi yalishirikisha askari na maafisa uhamiaji 507 yalikuwa ni moja ya hatua ya kupanda cheo.

Awali, Meja Jenerali Kingu alikagua vikosi na baadae Gwaride maalumu la kufunga mafunzo kutoka kwa wahitimu lilipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima za ambapo wananchi waliofika kushuhudia sherehe hizo walishangilia kwa nguvu na vigelegele wakifurahia gwaride hilo.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu akisalimiana na Mkuu wa  Shule ya Polisi pamoja na wakufunzi wa shule hiyo.
Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Mrakibu Mwandamizi Bazo akisalimiana na Katibu Mkuu Meja Jenerali Kingu

Mgeni rasmi Meja Jenerali Kingu na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala (kushoto) wakitoa heshima zao kwa gwaride.
Gadi ya Askari na Maafisa Uhamiaji likipita mbele ya mgeni Rasmi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya Upandishaji vyeo katika shule ya Polisi.


GAadi ya Askari na Maafisa wa kike ikiongozwa na  Mkufunzi Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Salma Panja likipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima zake.

27 Julai 2018

24 Julai 2018

KAMISHNA WA MAGEREZA ALIPOFANYA ZIARA YA KUJITAMBULISHA KWA CGI







Watumishi wa Uhamiaji waanza Mafunzo ya Usimamizi wa Vihatarishi


Baadhi ya Maafisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Makao Makuu wameanza mafunzo ya siku tatu juu ya Usimamizi wa Vihatarishi (Risk Management) katika jengo la Makao Maku ya Idara hiyo Kurasini jijini Dar es salaam.

Mafunzo hayo yanaratibiwa na Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Andrew Malyeta ambaye pia ni Mratibu wa Usimamizi wa Vihatarishi katika Idara hiyo amesema lengo kuu la mafunzo haya ni kuwapa uelewa watumishi  katika Usimamizi wa Vihatarishi kutokana na Muongozo wa Usimamizi wa Vihatarishi katika Sekta ya Umma (Guidelines for Developing and Implementing Institutiona Risk Management Framework in Public Sector, December 2013) pamoja na Sera ya Usimamizi wa Vihatarishi ya Idara ya Uhamiaji (Institutional Risk Management Framework and Guide for the Immigration Department, 2016).

 “Kwa muongozo na sera hio tunategemea maafisa wetu watajifunza mambo muhimu sana katika utendaji kazi wao wa kila siku ambayo ni Muundo wa Usimamizi wa Vihatarishi, Wadau wa Usimamizi wa Vihatarishi, Majukumu ya mabingwa wa Vihatarishi, Hatua za Usimamizi wa Vihatarishi, Mgawanyo wa Vihatarishi, rejesta za Viharatishi pamoja na Nyenzo zinazotumika katika Usimamizi wa Vihatarishi’’ aliongeza Mrakibu Msaidizi Malyeta.

Mafunzo haya yanafanyika kwa ushirikiano na wawezeshaji katika Usimamizi wa Vihatarishi kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bwana Josephat Kajonga ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi na Bi. Lulu Ishengoma ambaye ni Afisa kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi.

Jumla ya Watumishi (askari na kada ya kawaida) 20 wanahudhuria mafunzo haya kutoka vitengo vya Uhasibu, BMC, Manunuzi, Sheria, Mipango, Anuwai za Jamii na Utumishi.

Mwezeshaji kutoka NIDA Bw. Josephat Kajonga akielekeza jambo wakati wa Mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamsikiliza muwezeshaji





23 Julai 2018

ZIARA YA KAMISHNA JENERALI MIKOA YA KUSINI






Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akiongea na Maafisa Uhamiaji wa Msumbiji katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji mkoani Ruvuma katika kijiji cha Mkenda

19 Julai 2018

18 Julai 2018

Kamishna Jenerali awahakikishia raia wa Msumbiji na Tanzania usalama juu ya maisha yao

WAKIMBIZI KUTOKA MSUMBIJI WAHAKIKISHIWA USALAMA WAO.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dakta ANNA MAKAKALA amewahakikishia raia kutoka nchini Msumbiji ambao wamewasili katika kijiji cha KIVAVA wilaya ya Mtwara kwa madai ya kukimbia machafuko yaliyotokea nchini mwao watarejea kwao katika hali ya amani na usalama.

Raia hao ambao wako chini ya uangalizi wa serikali ya Tanzania tokea kuingia kwao Julai mwaka huu, walielezwa na Kamishna Jenerali Dakta MAKAKALA amesema kilichobaki hivi sasa ni kufanya mawasiliano na nchi yao ili kuona namna ya kuwarejesha. 

Akizungumza na raia hao kwa lengo la kuwajulia hali, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dakta ANNA MAKAKALA amewahakikishia kwamba watarejea nchini mwao wakiwa salama.

Hawa ni raia kutoka nchini Msumbiji ambao wameweka kambi katika kijiji cha KIVAVA wilaya ya Mtwara wakipatiwa huduma mbalimbali za kijamii na serikali ya Tanzania kwa madai ya kukimbia machafuko ambayo yametokea nchini mwao.

Tarehe kumi Julai 2018 serikali ilianza kupokea raia 544 wa kitanzania na raia 102 wa Msumbiji ambao wote hao walikuwa wanaishi nchini Msumbiji wakijishughulisha na kilimo.

SAID MANDANDA ni mmoja wa raia hao wa  Msumbiji kutoka kitongoji cha Mapondo kijiji cha Ujamaa Kisungule wilaya ya Palma na hapa anamueleza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dakta ANNA MAKAKALA ambaye amewasili katika kijiji cha KIVAVA kuzungumza na raia hao.



07 Julai 2018

Sabasaba Special

Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani akiwa katika Banda la Uhamiaji katika Maonesho ya 42 ya Dar es salaam, Sabasaba 2018.