Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Kangi Lugola kesho Jumamosi tarehe 31
Agosti anatarajiwa kufungua mkutano wa Maafisa Uhamiaji Waandamizi kutoka mikoa
ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Akitoa
taarifa hiyo mjini Moshi leo, Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu Mwandamizi
Alhaji Ally Mtanda amesema kuwa mkutano huo wa siku mbili chini ya Uenyekiti wa
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala utafanyika katika Chuo cha
Kikanda cha Uhamiaji (TRITA) mjini Moshi una lenga kujadili na kutathmini utendaji
kazi wa idara pamoja na kukumbushana masuala mbalimbali hususan Sheria, Kanuni
na Taratibu ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na raia wa kigeni.
“Mkutano
huu utahudhuriwa na Makamishna wa Uhamiaji, Maafisa Uhamiaji Mikoa yote Tanzania
na Zanzibar, Wakuu wa Vitengo pamoja na Wafawidhi wa Vituo vya Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid
Amani Karume (AAKIA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA),
Namanga, Tunduma na Bandari ya Zanzibar.” Aliongeza Alhaji Mtanda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni