Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

31 Machi 2022

Ziara ya CGI Dkt. Anna Makakala Mkoani Morogoro yafana sana

 Na. Konstebo Amani Mbwaga Morogoro.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala leo tarehe 22 Machi 2022 amefanya ziara ya kikazi Mkoani Morogoro ambapo amefanya kikao kazi na maafisa na askari wa Uhamiaji mkoani humo.

Dkt. Makakala alipowasili alipokelewa na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Joseph Kasike sanjari na kupatiwa salamu ya heshima kutoka katika gwaride la mapokezi la Jeshi la Uhamiaji Mkoani Morogoro na baadae kukagua utendaji kazi, kusaini kitabu cha wageni na kisha kuongea na vyombo vya habari kuhusu lengo la ziara yake Mkoani Morogoro na baadae kuendesha kikao kazi cha maafisa, askari na watumishi raia.

Akiongea katika kikao kazi hicho amesisitiza kuendelea kuzingatia suala la nidhamu, utii na uhodari katika kutekeleza majukumu ya Uhamiaji kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu kwa manufaa ya ulinzi na usalama wa nchi.

CGI Dkt. Makakala amewapongeza Maafisa na Askari wa Uhamiaji Mkoani hapo kwa kuwa waanzilishi wa kwanza wa kauli mbiu ya Uhamiaji na kuitekeleza kwa vitendo kauli mbiu hiyo ambayo ni "Uhamiaji Upendo Mshikamno Uwajibikaji na kukataa Rushwa"

Dkt. Makakala ameendelea kuupongeza Mkoa wa Morogoro kwa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu.

Aidha amewataka kuendeleza misako na doria ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu sambamba na utoaji wa elimu ya uraia na kuendeleza zoezi la kutambua walowezi nchi nzima.

Kwa upande wake Afisa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Joseph Kasike akitoa taarifa ya utendaji kazi ya Mkoa alisema Mkoa wa Morogoro una jumla ya Wilaya saba (07) ambazo ni Morogoro, Kilombero, Kilosa, Ulanga, Malinyi, Mvomero na Gairo ambazo kote huduma za kiuhamiaji zinapatikana.

SACI Kasike aliongeza kwamba Mkoa wa Morogoro umeendelea kupata mafanikio mengi zaidi ikiwemo kutoa elimu ya uraia kwa umma, kufungwa kwa mfumo wa hati za dharula za kielektroniki Wilayani Gairo, kupatiwa pikipiki mpya aina ya Honda Wilayani Mvomero ili kurahisisha doria na misako ya mara kwa mara.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni