Matangazo
23 Julai 2018
ZIARA YA KAMISHNA JENERALI MIKOA YA KUSINI
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akiongea na Maafisa Uhamiaji wa Msumbiji katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji mkoani Ruvuma katika kijiji cha Mkenda
19 Julai 2018
VIGEZO NA SIFA ZA KUPATA PASIPOTI MPYA YA KIELEKTRONIKI
Msikilize msemaji mkuu wa Idara ya Uhamiaji akieleza vigezo na sifa za mwombaji wa Pasipoti mpya ya Kielektroniki.
18 Julai 2018
Kamishna Jenerali awahakikishia raia wa Msumbiji na Tanzania usalama juu ya maisha yao
WAKIMBIZI KUTOKA MSUMBIJI WAHAKIKISHIWA USALAMA WAO.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dakta ANNA MAKAKALA
amewahakikishia raia kutoka nchini Msumbiji ambao wamewasili katika kijiji cha
KIVAVA wilaya ya Mtwara kwa madai ya kukimbia machafuko yaliyotokea nchini mwao
watarejea kwao katika hali ya amani na usalama.
Raia hao ambao wako chini ya uangalizi wa serikali ya Tanzania
tokea kuingia kwao Julai mwaka huu, walielezwa na Kamishna Jenerali Dakta
MAKAKALA amesema kilichobaki hivi sasa ni kufanya mawasiliano na nchi yao ili
kuona namna ya kuwarejesha.
Akizungumza na raia hao kwa lengo la kuwajulia hali, Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dakta ANNA MAKAKALA amewahakikishia kwamba
watarejea nchini mwao wakiwa salama.
Hawa ni raia kutoka nchini Msumbiji ambao wameweka kambi katika
kijiji cha KIVAVA wilaya ya Mtwara wakipatiwa huduma mbalimbali za kijamii na
serikali ya Tanzania kwa madai ya kukimbia machafuko ambayo yametokea nchini
mwao.
Tarehe kumi Julai 2018 serikali ilianza kupokea raia 544 wa
kitanzania na raia 102 wa Msumbiji ambao wote hao walikuwa wanaishi nchini
Msumbiji wakijishughulisha na kilimo.
SAID MANDANDA ni mmoja wa raia hao wa Msumbiji kutoka kitongoji cha Mapondo kijiji cha Ujamaa Kisungule wilaya ya Palma na hapa anamueleza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dakta ANNA MAKAKALA ambaye amewasili katika kijiji cha KIVAVA kuzungumza na raia hao.
07 Julai 2018
Sabasaba Special
Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani akiwa katika Banda la Uhamiaji katika Maonesho ya 42 ya Dar es salaam, Sabasaba 2018.
05 Julai 2018
04 Julai 2018
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)



