
Ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya ofisi ya uhamiaji Mkoa wa Mtwara mara baada ya Kamishina Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala kufanya mabadiliko madogo ya uongozi ndani ya Mkoa huo ambapo amemuhamisha Kamishina Msaidizi James A. Mwanjotile kwenda Jijini Dodoma Kuwa Afisa Uhamiaji Mkoa kuchukua nafasi ya aliyekua Afisa Uhamiaji jijini hapo Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACI) Abdallah Kitimba ambae amestaafu kazi kwa mujibu wa sheria.
Mabadiliko hayo yameambatana na uteuzi wa Afisa Uhamiaji mpya wa Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi Novati Kato ambaye awali alikuwa Afisa Uhamiaji Msaidizi Mkoa wa Morogoro.
Akikabidhi Ofisi, Rasilimali watu na vifaa Kamishina Msaidizi Mwanjotile amewashukuru maofisa na askari wa Mkoa huo kwa kumpa ushirikiano wa kutosha kwa kipindi chote alichoongoza Mkoa huo na kuwataka kuendeleza ushirikiano huo kwa kiongozi mpya aliyewasili kuchukua nafasi yake.
Kamishina Msaidizi James A. Mwanjotile anaondoka Mkoa wa Mtwara akiwa amehudumu kwa kipindi cha miaka mitatu (3) Kwa nafasi hiyo ya Afisa Uhamiaji Mkoa na kuleta na mafanikio makubwa sana kwa Taifa, kutokana na Uongozi wake imara wenye Utii, Uhodari na Weledi wa hali ya juu.
HABARI PICHA NA MATUKIO
![]() |
Kaimu Afisa Uhamiaji Wilaya ya Tandahimba Mkaguzi Msaidizi Raymund Mapunda (Aliyesimama) akitoa maelezo ya awali kuhusu kituo cha Uhamiaji wilayani hapo |
![]() |
Makabidhiano ya Ofisi za Vituo Mbalimbali vya Uhamiaji yakiendelea |
![]() |
Mfawidhi wa Kituo cha Uhamiaji Kilambo Mkaguzi Nestori Riwa (Kushoto) akitoa maelezo ya kituo wakati wa Makabidhiano kituo hicho kipo Wilaya ya Mtwara Vijijini Mkoani Mtwara |
![]() |
(Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Mtwara) |