Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Christina S. Mndeme mapema wiki hii amefanya ziara ya kutembelea vipenyo vya mkoa Ruvuma kukagua utayari wa Idara ya Uhamiaji na vyombo vya ulinzi na Usalama kwa ujumla katika kukabiliana na wahamiaji haramu hasa wakati huu wa Mapambano dhindi ya ugonjwa w Covid -19 unaosababishwa na Virusi vya Corona.
Ziara hiyo imemfikisha Mkuu wa Mkoa na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama Wilayani Nyasa katika kipenyo cha Chiwindi kinachopakana na nchi jirani ya Msumbiji.
Lengo kuu la ziara hiyo kufanyika ilikuwa ni kujiridhisha na ulinzi na usalama mipakani ili kudhibiti matukio yoyote yanayoweza kutokea hasa wakati huu ambapo wengi wanaweza kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya kihalifu kama vile matishio ya kiusalama (ugaidi), usafirishaji wa wahamiaji haramu kwa njia za (Panya) vipenyo nk.
Aidha Mhe. Mndeme ameipongeza Idara ya Uhamiaji kwa kufanya kazi zake kwa makini katika mipaka hiyo na kusisitiza kuendelea kufanya doria za mara kwa mara na kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha ulinzi na usalama wa Mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla unaimarishwa wakati wote.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo ya mipakani kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa pale wanapoona wageni wasiowafahamu kuingia chini au wanapoona vitendo viovu vyovvote vinapotokea ambavyo ni kinyume na sheria basi watoe taarifa, kwani jukumu la kuilinda nchi ni la kila Mtanzania.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni