Na Konstebo Amani Mbwaga, Dodoma
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji Tanzania IOM leo tarehe 26 Januari 2022 limekabidhi Pikipiki 03 aina ya Honda XL kwa ajili ya kusaidia huduma za Ki-Uhamiaji.
Katibu Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji Dkt. Qasim Sufi amemkabidhi Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala piki piki hizo pamoja na vifaa vingine ikiwemo makoti ya mvua, viatu vya mvua na radio za mawasiliano.
Makabidhiano hayo yamefanyika kwa kukabidhiana vifaa na hati za makabidhiano katika ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu iliyopo Jijini Dodoma
Dkt. Makakala amewashukuru IOM kwa kuendelea kushirikiana na Uhamiaji katika masuala mbalimbali ya Ki-Uhamiaji.
Aidha amewataka Maofisa na Askari kutumia vifaa hivyo vyema na kuvitunza vizuri ili viweze kusaidia katika utekelezaji wa majukumu ya Uhamiaji na Taifa kwa ujumla.
Katibu Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM Tanzania Dkt. Qasim Sufi akikabidhi vifaa hivyo amesema IOM itaendelea kushirikiana na kuendeleza uhusiano uliopo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae!
HABARI PICHA NA MATUKIO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni