Matangazo

📢 IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA — KARIBU KWENYE BLOG RASMI   ✦   📰 UHAMIAJI HABARI BLOGU — TUNAKULETEA MATUKIO KILA SIKU   ✦   📲 FUATA IDARA YETU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII   ✦   ✉️ WASILIANA NASI: info@immigration.go.tz   ✦   ☎️ +255-22-2850575/6

04 Juni 2018

UZINDUZI WA PASIPOTI ZA KIELEKTRONIKI MKOA WA KUSINI PEMBA

Hafla ya Uzinduzi wa Huduma za Pasipoti za Kielekroniki katika ofisi za Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba ambayo ilifanyika siku ya tarehe 31/05/2018 ilihudhuriwa na Mgeni Rasmi Mhe. Mohamed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba na viongozi mbali mbali wa Serikali ilifanyika katika Ofisi za Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba mjini Chakechake.

Mgeni rasmi Mheshimiwa Mohamed Abood katika hotuba yake alisisitiza sana raia kuleta nyaraka sahihi wanapokuja kuomba  pasipoti ili kurahisisha zoezi la utoaji wa pasipoti hizo, kuwataka kuacha kufoji nyaraka ili ili kuepuka kutofautiana kwa taarifa muhimu zinazotakiwa.

Pia alikemea utumaji wa mawakala ambao ni mianya ya rushwa, na watakaogundulika  aidha raia au afisa uhamiaji basi wananchi watoe taarifa kwa Kamishna wa Uhamiaji. Na ikiwa Afisa Uhamiaji anatuhumiwa, Mheshimiwa Abood alimtaka Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu amsimamishe kazi mara moja na kupisha uchunguzi juu yake.

Mheshimiwa Abood alimaliza kwa kuwataka wananchi wanaopewa pasipoti hizo kuzitunza kwani ikipotea gharama ya kuomba inaongezeka na aliwataka kuzitumia kwa dhumuni husika na sio kuzitupa hovyo.

Hafla hiyo ilimalizika kwa ugawaji wa pasipoti kwa viongozi mbalimbali waliohudhuria.




Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba akionesha pasipoti yake

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Kusini Pemba

Mhe. Mohamed Abood akipata maekelezo ya hatua za uchuakuaji wa taarifa za mteja kielekroniki






Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na maafisa na askari wa Uhamiaji wa ofisi ya Mkoa wa Kusini Pemba























Mgeni rasmi akiangalia namna ya uchukuaji wa taarifa za kibaiometriki kwa mteja unavyofanyika







Mwananchi na Mkazi wa Kusini Pemba akikabidhiwa pasipoti yake ya kielektroniki na Mheshimiwa Abood


25 Mei 2018

Uzinduzi wa Huduma za e-Passport Mkoa wa Dar.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Injinia Evarist Ndikilo leo amezindua rasmi Huduma za Utoaji wa Pasipoti ya Kielektronikia katika Mkoa wa Dar es salaam.

Hafla hiyo ya Uzinduzi ambayo ilifanyika katika Viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa, viongozi wa Dini na wananchi kwa ujumla ambapo pamoja na uzinduzi pia walipewa elimu kuhusu pasipoti hio mpya.

Mheshimiwa Injinia Ndikilo alisifu Idara ya Uhamiaji kwa hatua inazochukua katika kuboresha huduma zake kwa wananchi na wageni na aliwataka wananchi kuzitunza pasipoti hizi pindi wanapopatiwa.

”Kabla ya kuhitimisha hotuba yangu, napenda kutoa rai kwa wananchi wote watakaopata Pasipoti hizi za kielektronikia kuhakikisha kwamba wanazitunza vizuri ili zisiangukie mikononi mwa wahalifu. Tambueni ya kwamba, mtu ambaye atapoteza pasipoti hii itamgharimu kulipia Tsh. 500,000/= (kwa atakayepoteza mara ya kwanza) na Tsh. 750,000/= kwa atakayepoteza mara ya pili.” Alisisitiza Mheshimiwa Ndikilo.

Awali Kamishna wa Uhamiaji Pasipoti na Uraia Kamishna Kihinga alieleza kuwa Uzinduzi huu wa leo ni muendelezo ambapo siku kadhaa zilizopita Huduma kama hii ilizinduliwa mkoani Dodoma, ambapo pia Kamishna Kihinga alieleza kuwa hadi kufikia Julai mwaka huu mikoa yote itakuwa tayari imefungwa vifaa vya e-passport.

”Kwa sasa tumeanza kufunga mfumo wa utoaji huduma hizi Mikoani, ambako tumeshaanza kutoa huduma hii katika Jiji la Dodoma, na leo tutaanza kutoa huduma hiyo ya pasipoti katika Ofisi ya Mkoa wa Dar Es Salaam baada ya Mhe. Mgeni rasmi kutuzindulia. Aidha tunatarajia mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu tutakuwa tumekamilisha kufunga Mifumo ya utoaji huduma ya pasipoti mpya Mikoa yote, na hivyo huduma hiyo kutolewa nchi nzima.” Alieleza Kamishna Kihinga.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Sophia akiongea na Kamishna wa Pasipoti na Uraia

Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es salaam akimsikiliza kwa makini mkuu wa Wilaya ya Ilala


Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salum akisalimia na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam Naibu Kamishna wa Uhamiaji Crispin Ngonyani wakati wa Uzinduzi wa Huduma za e-Passport

Kamishna wa Uhamiaji Pasipoti na Uraia (Kamishna) Kihinga akimpokea mgeni Rasmi Kaimu Mku wa Mkoa wa Dar na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Injinia Evarist Ndikilo



Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Sophia akimsindikiza Mgeni Rasmi