Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

30 Desemba 2021

UHAMIAJI Yamshukuru Rais Samia Baada ya Kutunukiwa Nishani kwa Mara ya Kwanza Tangu Uhuru

 Na Konstebo Amani Mbwaga, Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Mhe. Samia Suluhu Hassan amewatunuku Nishani Maofisa na Askari wa Uhamiaji 25 ikiwa ni historia kwa mara ya kwanza kutokea tangu Uhuru.

Akitoa salamu wakati wa hafla ya uvalishaji nishani kwa maafisa na askari hao Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala alianza kwa kumshukuru Mungu na kisha kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusaini sheria ya kuifanya uhamiaji kuwa Jeshi na hatimae kustahili kupata nishani ambazo zimekuwa zikitolewa kwa majeshi mengine kwa muda mrefu.

“Kwa mantiki hiyo hafla hii ni ya kwanza katika historia ya Jeshi letu hivyo tuna sababu ya kushukuru na kuenzi tunu hii” alisema Dkt. Makakala

Aidha Kamishna Jenerali Dkt. Anna Makakala amewapongeza maafisa na askari waliovalishwa nishani ambapo kimsingi zimetolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo yeye kama mkuu wa chombo cha ulinzi na usalama kwa mamlaka aliyokasimishwa na Rais chini ya kifungu cha 9 (1) cha sheria ya Uhamiaji sura 54 ikisomwa pamoja na kanuni ya 156 (2) ya kanuni za uendeshaji za uhamiaji amewavalisha kwa niaba yake.

Akihitimisha hotuba yake Dkt. Makakala alisema kwa uzito wa tunu waliyopatiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyonayo chini ya kanuni ya 156 (1) ya kanuni za uendeshaji za Uhamiaji za mwaka 2018 inatupasa maofisa na askari kuzitendea haki kwa kuwajibika zaidi na kutekeleza majukumu kwa weledi, ari na uadilifu wa hali ya juu sanjari na kuzingatia sheria, kanuni taratibu na miongozo inayosimamia kazi za uhamiaji.

Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru ilitolewa kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala ambae alivishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es salaam  tarehe 09 Disemba 2021 wakati wa kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru, wengine ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu ambae alivishwa na Kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini kwa niaba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu sanjari na Naibu Kamishna wa Uhamiaji Albert Rwelamila, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Nasra Juma Mohamed na Mrakibu wa Uhamiaji Issa Mlweta Issa.

Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema ilitolewa kwa Mkaguzi wa Uhamiaji Kanyakula Titus Mrefu, Mkaguzi Wing Mombaka Said, Mkaguzi Hermina Azza Foya, Mkaguzi Emma Alex Kalyembe, Mkaguzi Beatrice Elineema Nyange, Mkaguzi Dkt. Clement Bernado Mubanga,  Mkaguzi Othman Khamis Ali, Mkaguzi Fikirini Abdallah Ali, Mkaguzi ABubakary Muhozi Yunusu, Mkaguzi Pilli Ally Mazige, Mkaguzi Msaidizi Gloria Godfrey Shayo,  Mkaguzi Msaidizi Jane Deusdedit Luhaga, Mkaguzi Msaidizi Zahra Abdu Akida, Mkaguzi Msaidizi Salma Mahboob Mkadar, Stafu Sajini Mbaraka Yusuph Ayoub, Stafu Sajini Bahati Jamali Ramadhani, Stafu Sajini Seif Abdullatif Khamis, Stafu Sajini Juma Omar Suleiman, Sajini Nyambeho John Siwa na Konstebo Stephano Aram Kayaga.

 HABARI PICHA NA MATUKIO

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru Naibu Kamishna wa Uhamiaji Nasra Juma Mohamed katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam



Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru Naibu Kamishna wa Uhamiaji Albert Rwelamila katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam



Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru Mrakibu wa Uhamiaji Issa Mlweta Issa katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akitoa Nasaha na Maelekezo kwa Maafisa Askari na Watumishi raia wa Uhamiaji mara baada ya kutunuku Nishani  katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam 

Mkuu wa Kitengo cha Utumishi Uhamiaji Makao Makuu ACI James Mwanjotile akitoa maelezo mafupi kuhusu Nishani wakati wa hafla ya uvalishwaji Kurasini Jijini Dar es salaam


Kamishna wa Uhamiaji Fedha na Utawala Hamza Shabani

Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Pasipoti na Uraia Gerald Kihinga (Kulia)

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akizungumza na vyombo vya habari baada ya hafla ya kuvisha Nishani kwa Maofisa na Askari wa Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam




Picha ya Pamoja Maofisa na Askari



Picha ya Pamoja na Brass Band ya Polisi

Picha ya Pamoja na Uhamiaji Tanzania Band

Picha ya Pamoja na NCOs waliovishwa Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema







Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Konstebo wa Uhamiaji Stephano Aram Kayanga  katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Sajini Nyambeho John Siwa katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Stafu Sajini Seif Abdulatif Khamis katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Stafu Sajini Bahati Jamali Ramadhani katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Stafu Sajini Mbaraka Yusuph Ayoub katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Mkaguzi Msaidizi Salma Mahboob Mkadar  katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Mkaguzi Msaidizi Zahra Abdu Akida katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam




Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Mkaguzi wa Uhamiaji Pili  Ally Mazige katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam






Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Mkaguzi wa Uhamiaji Dkt. Clement Bernado Mubanga katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala akimvisha Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu na Tabia Njema Mkaguzi wa Uhamiaji Beatrice Elineema Nyange  katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam








Mfawidhi Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl, Nyerere (JNIA) Naibu Kamishna wa Uhamiaji Albert Rwelamila akiteta jambo na Msemaji Mkuu wa Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle wakati wa hafla ya uvalishaji wa Nishani iliyofanyika Kurasini Jijini Dar es salaam (Picha zote na Konstebo Amani Mbwaga Uhamiaji Makao Makuu)

24 Desemba 2021

Sikukuu njema ya Krismasi kwa Watanzania Wote


 

"Kwa niaba ya Maafisa, Askari na Watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji, Nawatakia Watanzania wote Sikukuu Njema ya Krismasi. Tusherehekee kwa amani na utulivu ili tuweze kufika salama mwaka 2022" - Dkt. Anna Makakala

20 Desemba 2021

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamaji yalivyofana Dodoma Naibu Waziri Chilo atoa neno

Na Konstebo Amani Mbwaga, Dodoma

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Khamis Hamza Chilo ameongoza maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya wahamaji ambayo hufanyika kila tarehe 18 Disemba ya kila mwaka, ambapo mwaka huu maadhimisho hayo yamefanyika Jijini Dodoma katika viwanja vya Mwl. Nyerere.

Mhe. Chilo akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alisema Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani katika kutambua umuhimu wa mchango wa haki wanazostahili wahamaji ndio maana mwaka huu maadhimisho hayo yamekwenda kwa kauli mbiu isemayo “Kutumia fursa za uhamiaji wa binadamu”

Siku ya wahamaji ilianza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza duniani mwaka 2000 baada ya kutangazwa na mkutano mkuu wa umoja wa mataifa (UN General Asembly) tarehe 04 Disemba 2000 kupitia azimio hilo masuala yote yanayotambua umuhimu wa mchango na haki wanazostahili wahamiaji duniani yalipewa kipaumbele.

“Tunahitaji kuzitumia fursa za Ki-Uhamiaji kwa binadamu ili kuweza kufikia malengo yetu” alisema Mhe. Chilo

Aidha ametoa wito kwa Uhamiaji kuendeleza doria, misako na operesheni mbalimbali katika maeneo yote ya mipaka ya nchini.

"Nendeni mkaendeleze kwa sababu najua kazi huko inaendelea ya misako na doria ya kupambana na kuwasaka wahamiaji haramu lakini nendeni mkaendeleze jitihada hizi ili lengo na madhumuni tuishi kwa amani na usalama” alisema

Kwa upande wake mwakilishi wa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini ambae pia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu alisema tangu tarehe 15 Disemba 2021 Jeshi la Uhamiaji lilianza maadhimisho hayo kwa kuwa na maonesho ya huduma mbalimbali za kiuhamiaji sambamba na kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya uraia, pasipoti, visa, vibali vya ukaazi sanjari na masuala ya wahamiaji haramu.

“Tanzania kama ilivyo nchi mbalimbali duniani imeendelea kutumia fursa za wahamaji hususani wale wanaoingia nchini kwa kufuata sheria kanuni na taratibu za nchi, kundi hili ni muhimu sana katika katika maendeleo ya Taifa letu" alisema Kamishna Sururu.

Aliongeza Pamoja na kutumia fursa za uhamiaji wa kibinadamu Jeshi la Uhamiaji limeendelea kudhibiti wahamiaji wasio rasmi na ambao hawafuati sheria na taratibu za nchi wakati wa kuingia na kutoka nchini.

Lengo la udhibiti huo ni kuhakikisha nchi inakua salama wakati wote ili kuepukana na ujambazi, ugaidi, utakatishaji fedha na usafirishaji haramu wa binadamu.

Maadhimisho ya siku hiyo yalihudhuriwa na Wakuu wa Uhamiaji Wastaafu akiwemo Mkurugenzi wa Uhamiaji (Mstaafu) Kinemo Kihomano aliyeoongoza Uhamiaji kutoka mwaka 1997 hadi mwaka 2010, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji (Mstaafu) Magnus Ulungi aliyeongoza Uhamiaji toka mwaka 2010 hadi 2013 na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji (Mstaafu) Sylvester Ambokile aliyeongoza Uhamiaji toka mwaka 2013 hadi mwaka 2015.

Siku hiyo ya Kimataifa ya Wahamaji ilihitimishwa kwa mgeni rasmi Mhe. Naibu Waziri Chilo kukagua mabanda ya maonesho ya shughuli za kiuhamiaji na banda la IOM-Tanzania sanjari na kukutana na bendi ya Uhamiaji iliyotumbuiza katika siku hiyo ambapo aliipongeza sana kwa kuendelea kutoa burudani na elimu kwa umma juu ya masuala ya Kiuhamiaji.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Khamis Hamza Chilo (katikati) akipokea maandamano ya maafisa askari na watumishi rai wa uhamiaji katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamaji iliyofanyika Jijini Dodoma katika uwanja wa Mwl. Nyerere tarehe 18 Disemba 2021

Wawakilishi wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama


Maandamano ya maaofisa askari na watumishi raia wa Uhamiaji wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya wahamaji jijini Dodoma





Kamishna Mkuu wa Uhamiaji (Mstaafu) Sylvester Ambokile 

Kamishna Mkuu wa Uhamiaji (Mstaafu) Magnus Ulungi 

Kamishna Mkuu wa Uhamiaji (Mstaafu) Sylvester Ambokile kushoto akiteta jambo na Kamishna wa Uhamiaji anaeshughulikia Huduma za Sheria Kamishna Edmund Mrosso katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya wahamaji tarehe 18 Disemba 2021





Mkurugenzi wa Uhamiaji (Mstaafu) Kinemo Kihomano (Kulia) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Anuai za Jamii Uhamiaji Makao Makuu Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mwanahamis Kawina katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wahamaji iliyofanyika jijini Dodoma





Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Khamis Hamza Chilo (Kushoto) akiteta jambo na Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Vibali vya Ukaazi Pasi na Visa  Marry Palmer ndc katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya wahamaji iliyofanyika tarehe 18 Disemba 2021, Jijini Dodoma katika viwanja vya Mwl. Nyerere.





Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Khamis Hamza Chilo (katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Mrakibu wa Uhamiaji Azizi Kirondomara kuhusu huduma za kiuhamiaji katika banda la maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamaji iliyofanyika Jijini Dodoma katika uwanja wa Mwl. Nyerere tarehe 18 Disemba 2021



















Brass Band ya Makutupora JKT ikiongoza maandamano ya maofisa askari na watumishi wa uhamiaji katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya wahamaji tarehe 18 Disemba 2021 Jijini Dodoma



(Picha zote na Konstebo Amani Mbwaga)

#DAKIKA 45 ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WAHAMAJI DISEMBA 2021 ...