Matangazo
29 Machi 2018
26 Machi 2018
ANATAFUTWA
NDG. FAISALI HIRARY MWENYE PICHA HAPO JUU ANATAFUTWA NA
IDARA YA UHAMIAJI KWA KOSA LA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU KINYUME NA KIFUNGU
CHA 46 CHA SHERIA YA UHAMIAJI, SURA YA 54, REJEO LA MWAKA 2016.
YEYOTE
MWENYE TAARIFA KUHUSU MTUHUMIWA HUYO, ANAOMBWA KUIFIKISHA KATIKA OFISI YOYOTE
YA UHAMIAJI AU KITUO CHA POLISI KILICHO KARIBU NAYE.
AIDHA,
TAARIFA INAWEZA KUTOLEWA KWA NJIA YA SIMU KUPITIA NAMBA IFUATAYO: 0768
636 505.
“Pamoja Tushirikiane Kuilinda Nchi Yetu”
-------------------------
IMETOLEWA
NA
KITENGO CHA UHUSIANO,
IDARA
YA UHAMIAJI,
MAKAO MAKUU,
16 Machi 2018
07 Machi 2018
ELIMU KWA UMMA SINGIDA YAZAA MATUNDA, WATUHUMIWA SITA WAKAMATWA
Idara ya Uhamiaji Mkoani Singida
imetoa elimu kwa Umma kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Idara ya
Uhamiaji zikiwemo Pasipoti, Vibali vya Ukaazi,Uraia na Uhamiaji haramu. Zoezi
hilo linaendelea kufanyika katika Wilaya zote Sita za mkoa wa Singida ambazo ni Manyoni, Mkalama, Ikungi, Iramba,
Singida Mjini na Vijijini.
Katika kutekelaza zoezi hilo
Maafisa Uhamiaji Wilaya wanashirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya
husika pamoja Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa/Vitongoji mbalimbali ikiwa ni
lengo la kuwajengea uelewa Viongozi hao kuhusu masuala yanayohusu Uhamiaji.
Sambamba na elimu kwa umma,
Uhamiaji Singida wameimarisha Mapambano ya Wahamiaji haramu kwa kufanya misako
na doria za mara kwa mara katika maeneo yanayozaniwa kuwa hifadhi ya Wahamiaji
haramu.
“Mpango huu wa Elimu kwa Umma umesaidia
kufanikisha kuwakamata Wahamiaji haramu [02] Raia wa Ethiopia pamoja na Watanzania [04]
ambao wanajihusisha na biashara haramu ya kusafirisha Wahamiaji haramu, Watuhumiwa
wote wamefikishwa Mahakamani. Wananchi wamekuwa na mwamko na wamesaidia katika kuwaafichua watuhumiwa hao. Natoa rai kwa Wananchi kuendelea kushirikiana na Idara ya
Uhamaji kwa kutoa taarifa kwa Vyombo vya ulinzi na usalama pale wanapobaini
kuna mtu au kikundi cha watu wanaodhaniwa kuwa wahamiaji haramu’’ alizungumza
Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoa Singida, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Angela M. Shija.
Katika zoezi hilo kwa Wilaya ya
Iramba inaongozwa na Kaimu Afisa Uhamiaji Wilaya Mkaguzi Dotto Selasini na kwa Wilaya
za Singida Mjini na Vijijini linaratibiwa na kusimamiwa na Wakaguzi Wasaidizi
Lawi Kumburu na Marcelin Marwa. Fuatilia habari picha zifuatazo:-
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Lwehaula (aliyeshika kitabu) akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya katika mkutano ambapo Kaimu Afisa Uhamiaji alipata fursa ya kutoa elimu kwa Umma.
|
![]() |
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kidaru waliohudhuria mkutano ambapo walipata elimu katika masuala mbalimbali yanasimamiwa na Idara ya Uhamiaji.
|
![]() |
Wanakijiji wa Kidatu wakifuatilia kwa makini Elimu juu wa Wahamiaji Haramu iliyokuwa ikitolewa na Mkaguzi wa Uhamiaji Dotto Selasini
|
06 Machi 2018
Uhamiaji walipotia 'Mguu' Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala cha jijini Dar
Ukaguzi wa uhalali wa Ukaazi wa watumishi wa chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala uliofanywa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akiwa na Mheshimiwa Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako chuoni hapo Gongolamboto jijini Dar es salaam.
05 Machi 2018
24 Februari 2018
UHAMIAJI YASHIRIKI USAFI NA KUTOA ZAWADI KWA WANAFUNZI KATIKA SHULE YA MSINGI MATUMAINI JIJINI DAR ES SALAAM.
Idara
ya Uhamiaji imeshiriki zoezi la kufanya usafi katika shule ya msingi Matumaini iliyoko Kurasini jijini Dar
es salaam. Shule hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Wokovu inasomesha wanafunzi
wenye mahitaji maalum toka Mikoa mbalimbali nchini na hata nje ya nchi.
Akiongea
kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Kamishna wa Utawala na Fedha,
Edward Peter Chogero ambaye ndiye aliyeongoza Maafisa, Askari na Watumishi wa
kada nyingine wa Idara hiyo, alisema zoezi hilo ni mwendelezo wa utekelezaji wa
agizo la Serikali la kufanya usafi katika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Aidha, Idara ya Uhamiaji ilitoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi wa shule hiyo
walio na mahitaji maalum ikiwa ni sehemu ya kuwafariji na kuwaonesha upendo ili
wajisikie ni sawa na watu wengine katika jamii.
Akiongea
kwa niaba ya Uongozi, Luteni Thomas Sinana ambaye ni Mkurugenzi wa Shule hiyo
aliishukuru na kuipongeza Idara ya Uhamiaji kwa moyo wa upendo waliouonesha kwa
wanafunzi hao wenye mahitaji maalum, kwa kushiriki kwao katika kufanya usafi
katika maeneo mbalimbali ya shule hiyo pamoja na kutoa zawadi mbali mbali kwa
watoto hao.
Luteni
Sinana alisema “kituo kina mahitaji mengi japo kuwa tunashirikiana na Serikali
kutoa elimu kwa vijana hawa kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba ila watoto
wote waliopo hapa wana mahitaji maalumu kutokana na ulemavu wao hivyo tunapopata
vifaa kama hivi vinatusaidia sana kwenye kituo chetu” .
Mwisho
watoto hao walipata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao mbalimbali ikiwa ni pamoja
na kazi za mikono wanazotengeza wenyewe, kuimba, kucheza na kuigiza.
| Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha) Edward Chogero akikabidhi zawadi kwa Kiranja Mkuu wa Shule ya Matumaini Ernest Thomas mara baada ya zoezi la kufanya usafi kumalizika shuleni hapo. |
| Maafisa Uhamiaji wakifanya usafi katika Shule ya Msingi Matumaini leo Jumamosi Februari 24, 2018 |
| Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Matumaini wakifuatilia tukio la kukabidhiwa zawadi |
| Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha) akiwa na Mkurugenzi wa Shule ya Matumaini Luteni Thomas Sinana |
| Kikundi cha Sanaa cha Shule ya Msingi Matumaini kikitumbuiza wakati wa zoezi la utoaji zawadi shuleni hapo |
| Wanafunzi wa Shule ya Msingi Matumaini wakitoa burudani kwa Maafisa Uhamiaji waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kushiriki usafi na kutoa zawadi |
| Wanafunzi wakisoma vipeperushi vyenye kuelezea maana ya Uhamiaji Mtandao |
| Kamishna Edward Chogero akiangalia vitu mbalimbali vinavyotengezwa na wanafunzi wa shule ya msingi Matumaini |
| Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Matumaini ambaye pia ndiye kaka Mkuu wa shule hiyo akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake mara baada ya kukabidhiwa zawadi hizo. |
| Maafisa Uhamiaji wakiwasalimia wanafunzi wa Shule ya Matumaini |
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)













