Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala kesho Jumanne tarehe 17 Septemba, 2019 anatarajia kufunga Mafunzo ya Uongozi ya awamu ya nne kwa Maafisa 54 wa ngazi ya Wakaguzi Wasaidizi wa Uhamiaji ambao wamehitimu mafunzo hayo.
Akitoa taarifa hiyo Mjini Morogoro, Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Mrakibu Mwandamizi Alhaji Ally Mtanda amesema kuwa Mafunzo hayo yatafungwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala katika Chuo cha Magereza cha Gereza Kuu Kingolwira – Morogoro.
Sherehe hizo za ufungaji wa mafunzo hayo zitahudhuriwa na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (CI-Znz), Kamishna wa Uhamiaji, Utawala na Fedha Edward Peter Chogero (CI - A&F), Kamishna wa TRITA, Maurice Kitinusa (CI - TRITA), Afisa Uhamiaji Mkoa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Angela Mathew Shija (ACI) pamoja na Wakuu wa Vitengo mbalimbali kutoka Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni