Matangazo

📢 IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA — KARIBU KWENYE BLOG RASMI   ✦   📰 UHAMIAJI HABARI BLOGU — TUNAKULETEA MATUKIO KILA SIKU   ✦   📲 FUATA IDARA YETU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII   ✦   ✉️ WASILIANA NASI: info@immigration.go.tz   ✦   ☎️ +255-22-2850575/6

16 Novemba 2020

UHAMIAJI Iringa yatoa Elimu ya Uhamiaji kwa Jeshi la Akiba

Iringa – Tanzania


Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa chini ya Afisa Uhamiaji Mkoa Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACI Agnes Michael Luziga imeendelea kutoa elimu ya Kiuhamiaji katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa huo.

Lengo kuu la elimu hiyo ni kupambana na wimbi la wahamiaji haramu na kuwezesha kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu kupitia utekelezaji wa sheria na kanuni zilizopo  ili kulinda usalama wa Taifa na kukuza maendeleo ya Kiuchumi.

Utoaji wa Elimu hiyo ya Uhamiaji umefanyika katika Mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) yanayoendelea katika Viwanja vya Mlandege vilivyopo Iringa Mjini, ambapo zaidi ya Kuruti 79 wa Jeshi hilo wamepatiwa elimu ya kiuhamiaji, ikiwemo Uraia, Pasipoti, Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka ya Nchi.

Mafunzo hayo yaliendeshwa na Maafisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa yakiongozwa na Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji A/ISP Omaru Mohamed na Afisa Uhusiano Uhamiaji (M) Konstebo Mariam Simba.

Aidha Jukumu la Ulinzi na Usalama wa Taifa letu ni la Kila Mtanzania, Katika zoezi la kupambana na wahamiaji haramu, Wananchi wanaaswa kushiriki  kwa kutoa taarifa katika Ofisi za Uhamiaji pindi wanapokutana na mtu au kundi la watu ambao wanawatilia shaka  katika maeneo yao ya kazi  ama makazi yao ili kuwezesha idara kuchunguza na kubaini sababu za ujio wa shughuli zao hapa nchini.

 HABARI PICHA NA MATUKIO

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Omaru Mohamed  (Kushoto) Akitoa Elimu ya Kiuhamiaji kwa Kuruti wa Jeshi la Akiba Mkoani Iringa kushoto kwake ni Mkufunzi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Omaru Mohamed Akitoa Elimu ya Kiuhamiaji kwa Kuruti wa Jeshi la Akiba Mkoani Iringa


Afisa Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa Konstebo Mariam Simba akifundisha Moja ya Mada za Kiuhamiaji kwa Kuruti wa Jeshi la Akiba Mkoani Iringa (Hawapo Pichani)

Kuruti wa Jeshi la Akiba Mkoani Iringa wakipata elimu ya Kiuhamiaji



(Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa)

13 Novemba 2020

HABARI PICHA CGI Dkt. Anna Makakala Ahudhuria Ufunguzi wa Bunge la 12 Lililofunguliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Dodoma, Tanzania
Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Mapema Leo Hii amezindua rasmi Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadae kulihutubia Bunge na Taifa kwa Ujumla juu ya  Mpango Mkakati wa Serikali yake wa miaka mitano.

Katika Ufunguzi huo Uliofanyika Jijini Dodoma, Umehudhuriwa pia na Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, Waheshimiwa Mabalozi, Viongozi wa Dini Wakuu wa Vyombo ya Ulinzi na Usalama Nchini akiwemo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala.

Aidha Rais Dkt. Magufuli  Amesisitiza suala la Kudumisha Amani Umoja na Mshikamano na kuhakikisha Nchi inakuwa salama ili wananchi wake waweze kujiletea maendeleo na  kuchapa kazi, kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae


HABARI PICHA NA MATUKIO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini waliosimama Nyuma


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Makamu wa Rais Wastaafu na Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waiwa na Wenza wao waliosimama Nyuma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi vyama vya Siasa waliosimama Nyuma







Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya Mabalozi wa Nchi Mbalimbali  waliosimama Nyuma



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliosimama Nyuma






Picha na Wabunge Zikiendelea





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya Viongozi wa Dini waliosimama Nyuma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya Makatibu Wakuu waliosimama Nyuma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya Watumishi wa Bunge waliosimama Nyuma






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Akiagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini, baada ya Kumaliza Shughuli ya Uzinduzi wa  Bunge Dodoma
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Uslama Nchini wakipiga Saluti Kuagana na Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli 




Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala Akisalimiana na Mhe. Job Ndugai Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya Kumaliza Shughuli za Uzinduzi wa Bunge la 12 Jijini Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Salamu ya Heshima



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Gwaride





(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)