Mwaka Mmoja wa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala kuongoza Idara ya Uhamiaji , Mengi amefanya katika kuboresha utendaji kazi wa Idara hii nyeti nchini.
Matangazo
13 Februari 2018
10 Februari 2018
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akagua vituo vya mpakani mkoani Kilimanjaro
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala amefanya
ziara ya siku moja katika vituo vya mpakani mkoa wa Kilimanjaro ikiwa na lengo kukagua utendaji kazi wa maafisa na
askari wa Uhamiaji katika vituo hivyo.
Akiwa kituo cha Holili alikagua mpaka na kuongea na watumishi
wa Idara ya Uhamiaji kituoni hapo na kuwasisitiza kufanya kazi kwa weledi na
juhudi pia kujiepusha na vitendo vya rushwa. Pia aliwataka kuzidisha
doria na ukaguzi maeneo ya mipakani ili kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu.
Katika kituo cha Tarakea, Kamishna Jenerali alikagua mpaka na utendaji kazi katika kituo hicho na baadaye
kuongea na watumishi wa uhamiaji na vyombo vingine vya serikali vinavyofanya kazi katika mpaka huo na kuwataka kuwa na ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao mpakani hapo.
Pia Kamishna Jenerali alisisitiza watumishi wa uhamiaji kufanya kazi kwa weledi na kufuata sheria za nchi pia kujiepusha na vitendo vya rushwa, pia aliwataka kuongeza kasi ya kufanya doria maeneo yanayodhaniwa kuwa ni vipenyo vya wahamiaji haramu kuingia nchini.
Pia Kamishna Jenerali alisisitiza watumishi wa uhamiaji kufanya kazi kwa weledi na kufuata sheria za nchi pia kujiepusha na vitendo vya rushwa, pia aliwataka kuongeza kasi ya kufanya doria maeneo yanayodhaniwa kuwa ni vipenyo vya wahamiaji haramu kuingia nchini.
Akiwa katika mpaka wa Rongai, Kamishna Jenerali aliongea na wananchi na kuwataka kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama katika ulinzi wa mpaka huo na kuwasisisitiza kutoa taarifa za wahamiaji haramu badala ya kukaa kimya na kuangalia tu kwani wananchi waishio mipakani wanalo jukumu kubwa katika ulinzi wa mipaka katika maeneo wanayoishi,
Akiwa mjini Moshi, Kamishna Jenerali
alifungua mafunzo ya Ukaguzi wa nyaraka na kujenga uwezo kwa maafisa wa vyombo ya ulinzi na usalama katika masula ya Ugaidi yaliyoanza
tarehe 8 Februari 2018 katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini
Moshi.
| Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akipata maelezo kutoka kwa Mfawidhi wa Kituo cha Uhamiaji katika mpaka wa Tarakea |
| Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akisalimiana na Maafisa na Askari wa Uhamiaji katika kituo cha Uhamiaji Holili wakati wa ziara yake katika kituo hicho |
| Msemaji wa Idara Mrakibu wa Uhamiaji Ally Mtanda akiwa na Afisa Uhusiano wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Mkaguzi wa Uhamiaji Leslie Mbotta |
09 Februari 2018
Fahamu kuhusu Uhamiaji Mtandao na Pasipoti ya Kielektroniki.
Uhamiaji
Mtandao ni Nini?
Uhamiaji
Mtandao (e-Immigration) ni muunganiko wa Mifumo mbalimbali ambayo imesanifiwa
kufanya kazi kwa pamoja na kutoa taarifa kwa watumiaji na wadau wa huduma za
kiuhamiaji.
Lengo la
Uhamiaji Mtandao
Lengo
kuu la Uhamiaji Mtandao ni Kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Nchi yetu, Kudhibiti
ukusanyaji wa maduhuli ya serikali na kuimarisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji
kwa raia na wageni wanaoingia na kuishi hapa nchini kwa madhumuni mbalimbali.
Mfumo
wa Uhamiaji Mtandao, utawezesha;
Idara ya Uhamiaji kutoa
viza kielektroniki (e-Visa); ambapo
mgeni ataweza kuwasilisha ombi lake na kupata majibu kwa njia ya kielektroniki.
Mfumo huo pia utasaidia Serikali kupata taarifa sahihi za malipo ya viza na
kuchagiza ukuaji wa Sekta ya Utalii nchini.
Mfumo wa Udhibiti na Usimamizi wa
Mipaka Kielektroni (e-Border Management), Mfumo
utasaidia kudhibiti na kuwezesha uingiaji na utokaji wa raia na wageni nchini,
Sambamba na hilo, Mfumo utasaidia kuchuja wageni wasiotakiwa kuingia nchini na hivyo
kuimarisha ulinzi hususan katika maeneo ya mipakani na kuzuia ongezeko la
wahamiaji haramu nchini.
Mfumo wa utoaji wa Vibali vya
Ukaazi Kielektroniki (e-Residence Permit), Mfumo huu
utasaidia kuboresha usimamizi wa utoaji vibali kwani mwombaji atawasilisha
maombi yake kwa njia ya kielektroniki. Hii itasaidia kukuza Sekta ya Uwekezaji
nchini kwa maendeleo ya uchumi wa Nchi yetu.
Mfumo wa Utoaji wa Pasipoti kielektroniki
(e-Passport); Mfumo huu ambao ndio wa kwanza katika
utekelezaji wa Mradi wa Uhamiaji Mtandao, utawawezesha waombaji wa huduma ya
Pasipoti kuwasilisha maombi yao kwa njia ya kielektroniki (Online Passport
Application) kutoka mahali popote walipo, na kuweza kufuatilia (Track) maombi hayo
kielektroniki.
Pasipoti
hii mpya ya Kielektroniki imesheheni sifa zifuatazo:
1. Imewekwa Kifaa maalum chenye uwezo
wa kutunza taarifa za mmiliki wa pasipoti “Micro-Chip” na hivyo kufanya suala
la utunzaji wa Usalama za Pasipoti hizi kuwa wa hali ya juu
2. Vile vile uwepo wa “Micro-Chip”
katika Pasipoti ya kielektroniki, kunaifanya pasipoti hii kuwa ngumu kuibiwa au
kutumiwa na wahalifu au watu wanaojaribu kuficha utambulisho
3. Vile vile
uwepo wa “Micro Chip” katika pasipoti ya kielektroniki, kunaifanya pasipoti ya
hii kuwa ngumu kuibiwa au kutumiwa na wahalifu au watu wanaojaribu kuficha
utambulisho wao kwa kutumia pasipoti zisizo zao.
4.
Pasipoti hiyo
ina viwango vilivyopendekezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Usafiri
wa Anga (ICAO).
5.
Pasipoti
inatumia mfumo bora wa Utunzaji wa taarifa za mmiliki wa Pasipoti
kielektroniki, ambao hurahisisha utunzaji wa taarifa za mhusika, na kuondoaa
urasimu wa ufuatiliaji wa kumbukumbu za mmiliki pale anapotaka huduma nyengine
6. Pasipoti
hiyo ina uwezo wa kutunza kumbukumbu za kibailojia (Biometric features)
Faida za Pasipoti Mpya ya Kielektroniki
Pasipoti
hii mpya ina uwezo wa kuhifadhiwa katika Simu ya Kisasa (Smart Phone) na hivyo
kumuwezesha mwenye nayo kupata msaada wa Hati ya Dharura katika Ubalozi wowote
wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, pale anapopotelewa na
pasipoti hiyo awapo nje ya nchi ili aweze kurudi nyumbani.
Aidha, Pasipoti mpya ya Tanzania ya Kielektroniki ina muonekano
unaofanana na pasipoti za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na
faida zake ni nyingi;-
(i) Utambulisho wa
pamoja wa raia wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanapokuwa nchi
za nje na hivyo kurahisisha kupata msaada wa huduma za kikonsula (consular services)
inapobidi. Kwa mfano, kupata msaada wa kurejeshwa nchini kupitia balozi za nchi
wanachama wakati wa dharura, ikiwa sehemu husika haina ubalozi wa Tanzania.
(ii)
Raia
wa nchi wanachama kutambuana wanapokuwa nje ya nchi na hivyo kujenga umoja wa kikanda
kwa ngazi ya raia, wanapokuwa nje, kwani ni rahisi kupata msaada kwa jirani
kuliko mtu wa mbali.
![]() |
| Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionesha pasipoti yake baada ya kukabidhiwa na Mheshimiwa waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dkt. Mwigulu Mchemba. |
![]() |
| Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu akionesha pasipoti yake ya kielektroniki wakati wa uzinduzi wa pasipoti hizo kwenye Ofisi za Uhamiaji Makao Makuu, Kurasini jijini Dar es salaam. |
07 Februari 2018
HATUA ZA UJAZAJI FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI (MTANDAO).
HATUA ZA UJAZAJI FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI KWA NJIA YA
KIELEKTRONIKI (MTANDAO).
2. CHAGUA
PASSPORT
APPLICATION FORM;
3. CHAGUA
OMBI
JIPYA;
4. TIKI
KIBOKSI KUKUBALIANA NA MAELEKEZO;
5. JAZA
TAARIFA ZAKO KWA UKAMILIFU UKIFUATA MAELEKEZO NA MPANGILIO (FORMAT) KATIKA KILA
KIPENGELE;
NB:
BAADA YA MWOMBAJI KUKAMILISHA KUJAZA TAARIFA
ZAKE, ATAFAHAMISHWA YA KWAMBA USAJILI UMEKAMILIKA NA KUPATIWA NAMBA YA OMBI, AMBAYO NI MUHIMU
AIANDIKE PEMBENI NA KUIHIFADHI KWA KUMBUKUMBU ZA BAADAE. KISHA ATAPEWA NAMBA YA
KUMBUKUMBU YA MALIPO (CONTROL
NUMBER) NA KUTAKIWA KWENDA KULIPIA MALIPO YA AWALI (ADVANCE FEE) YA TSH 20,000.
BAADA YA KUKAMILISHA USAJILI, NA KUPATIWA NAMBA YA OMBI NA NAMBA YA KUMBUKUMBU (CONTROL NUMBER), UKURASA UTAONEKANA KAMA
IFUATAVYO:
INGIA KWENYE MENU YA M-PESA/TIGOPESA (*150*00#/*150*01#)
1. Bonyeza Namba 4 (Lipa kwa M-Pesa) - VODA
2. Bonyeza Namba 4 (Kulipia Bili) - TIGO
Kisha Weka/Ingiza Namba ya Kampuni
3. Ingiza Namba (888999)
4. Ingiza kumbukumbu Namba(Ingiza Control Number inayoanzia na 99109…….)
5. Ingiza kiasi (kama ulivyo elekezwa Mfano: 20,000 nk.)
6. Utapata Maelezo kuwa unalipa pesa NMB
7. Ingiza Namba ya Siri
8. Hakiki
9. Utapata Meseji toka M-Pesa/Tigopesa kama muamala umekubalika;
Utapata meseji kutoka kwenye mfumo Namba 15200
kama muamala umekubalika;
kama muamala umekubalika;
10. Mteja atatakiwa
kurudi katika OMBI LINALOENDELEA:
11. Kisha ataingiza
NAMBA YA OMBI/SIMU na NAMBA YA RISITI
Na hapo ataweza kupakua Fomu yake ya
Maombi
Ataiwasilisha Fomu hiyo katika Ofisi
ya Uhamiaji Makao makuu au Afisi Kuu Zanzibar
1. Jaza fomu ya malipo
ya kielectroniki;
2. Fuata maelekezo
kama yanavyojieleza kwenye fomu;
3. Utapata meseji toka
benki;
Utapata meseji toka
kwenye mfumo Namba 15200
kama muamala umekubalika.
05 Februari 2018
Wanasiasa, Wafanyabiashara na Watu Maarufu wafika Uhamiaji kujipatia pasipoti za kielektroniki
Baada ya Idara ya Uhamiaji kuanza rasmi kutoa pasipoti za kielektroniki, Baadhi ya Wafanyabiashara na wanasiasa wakubwa nchini wameanza kufika Makao Makuu ya Uhamiaji kupata pasipoti hizo. Miongoni mwa waliofika kujipatia pasipoti ni Wafanyabiashara maarufu nchini Mzee Reginald Mengi akiwa na mkewe pamoja na Mzee Said Salim Bakhresa.
Kwa upande wa wanasiasa, Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowassa alifungua pazia kwa wanasiasa waliofika Uhamiaji Makao makuu kujipatia pasipoti hizo za kisasa zenye usalama wa hali ya juu.
Akiongea mara baada ya kupatiwa pasipoti yake, Mzee Mengi alisema amefurahishwa na mabadiliko makubwa ya kiutendaji ambapo amefanya maombi na kupatiwa pasi ndani ya siku moja kitu ambacho awali hakikuwepo.
''Hii ni hatua kubwa sana kwa kweli, Uhamiaji mmejitahidi mno, mimi na mke wangu tumefanya maombi leo na kupata pasipoti zetu, hongereni sana kwa hili" alisema Mzee Mengi ambaye aliambatana na Mkewe Bi. Jacqueline.
Naye Mheshimiwa Lowassa alisifu juhudi zinazofanywa na Idara ya Uhamiaji kwenye dhana ya Uhamiaji Mtandao ambapo ampongeza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala kwa juhudi zake za kuifanaya Idara ya Uhamiaji kwenda sambamba na tekinolojia.
01 Februari 2018
TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KWA UMMA:
UFAFANUZI
JUU YA “UZUSHI” UNAOENEA KWENYE TOVUTI NA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU IDARA YA
UHAMIAJI KUTANGAZA NAFASI ZA KAZI.
Katika
siku za hivi karibuni, kumekuwepo na uvumi unaoenezwa kupitia baadhi ya tovuti
na mitandao ya kijamii kuhusu kutangazwa kwa nafasi za ajira na Idara ya
Uhamiaji kwa ngazi ya Mkaguzi Msaidizi, Koplo na Konstebo. Tunaamini uvumi huo unaenezwa na watu au kikundi cha watu kwa nia ya
kujipatia maslahi yao binafsi au kwa malengo wanayoyafahamu wao.
Kufuatia
kuwepo kwa taarifa hizo, Idara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
- Idara
ya Uhamiaji haijatangaza nafasi
zozote za ajira katika kipindi cha hivi karibuni, hivyo tunawaomba
wananchi wasirubuniwe au kushawishiwa na mtu yoyote kutoa kitu chochote
ili waweze kusaidiwa kupata kazi Idara ya Uhamiaji.
- Taarifa
za kutangazwa nafasi za kazi zilizotolewa kupitia blogu husika na Mitandao
ya kijamii si za kweli, bali ni
uzushi uliofanywa na watu au kikundi cha watu kwa malengo wanayoyajua wao.
- Idara ya Uhamiaji, kama Taasisi ya
Serikali hutangaza nafasi za ajira
kwa uwazi kupitia Magazeti, Televisheni na Tovuti yake ambayo ni
‘www.immigration.go.tz’
- Idara inalaani na kukemea vikali
watu au kikundi cha watu kinachotoa taarifa za upotoshaji kuhusu Idara
kutangaza nafasi za kazi kama ambavyo imeripotiwa kwenye baadhi ya tovuti
na mitandao ya kijamii.
Imetolewa
na;
KITENGO CHA UHUSIANO,
MAKAO MAKUU, DAR ES SALAAM.
TAREHE: 01 FEBRUARI, 2018
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)






