Usikose kutazama Kipindi cha Hamza Kassongo On Sunday kupitia TVE leo Usiku. #ePssport #eVisa #ePermit #eBorder
Matangazo
05 Agosti 2018
04 Agosti 2018
03 Agosti 2018
NANE NANE 2018
Mhashamu Baba Askofu Renatus Nkwande wa Dayosisi ya Bunda alipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji, katika Maonesho ya Kilimo (NaneNane), katika Uwanja wa Nyakibindi, mkoani Simiyu. #ePassport #ePermit #eVisa #eBorder
02 Agosti 2018
Naibu Waziri wa Kilimo atembelea Banda la Uhamiaji
Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa atembelea Banda la Uhamiaji kwenye Maonesho ya Kilimo (NaneNane) Uwanja wa Nyakabindi, Mkoani Simiyu
01 Agosti 2018
WACHEZAJI WA SOKA WA TIMU YA TAIFA UMRI CHINI YA MIAKA 13 WAKABIDHIWA PASI ZAO
Kamishna wa Uhamiaji (Uraia na Pasipoti) Kamishna Gerald Kihinga amekabidhi pasipoti mpya za kielektroniki 16 kwa wachezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa chini ya umri wa miaka 13 (U13) kutoka shule ya Fountain Gate.
Vijana hao wanatarajia kusafiri kwenda nchini Ubelgiji kushiriki mashindano ya Soka ya Dunia kwa vijana wa umri chini ya miaka 13.
Aidha, Kamishna Kihinga aliwapongeza vijana hao kwa kuiwakilisha nchi na kuwataka kucheza kwa juhudi ili walete kombe nchini.
"Leo tumewapatia pasipoti ili muweze kusafiri kwenda kwenye mashindano, pia nawapongeza sana kwa kuchaguliwa kwenu kuiwakilisha nchi yetu, hivyo nawaomba mkacheze kwa juhudi na moyo wa kizalendo ili mchukue kombe na kuiletea sifa nzuri nchi yetu" alisema Kamishna Kihinga.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)








