
Visitors
23 Machi 2021
11 Machi 2021
Hivi ndivyo Wanawake Uhamiaji Zanzibar walivyowafariji watoto yatima katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani
Zanzibar
Katika shamra shamra za kuadhimisha siku ya
wanawake duniani iliyofanyika tarehe 8 Machi ya kila mwaka wanawake wa uhamiaji
kwa kushirikiana na wafanyakazi wote wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar walitoa misaada
mbali mbali kwa watoto yatima ambao wanaishi katika mazingira magumu pamoja na
kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka kituo hicho.
Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Chiku Khamis Omar
alikabidhi misaada katika kituo cha watoto yatima kiitwacho Markaz Alyaqiin
Islamic Centre kilichopo Kinduni Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa niaba wanawake wa Idara ya
Uhamiaji Zanzibar.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi misaada hiyo
Kamishna Msaidizi Chiku amewashukuru viongozi wa watoto hao kwa kukubali
kupokea misaada hiyo na kuwaahidi kua wanawake wa Uhamiaji wataendelea kutoa
misaada zaidi kwa watoto hao kila hali itakaporuhusu.
Miongoni mwa misaada hiyo ni pamoja na mchele, sukari,
sabuni, vitakasa mikono na mipira ya kuchezea.
Nae kiongozi wa kituo hicho Maalim Adam Bakar Haji
ambae ni kaimu Mwenyekiti wa kituo hicho amewashukuru wanawake wa Idara ya
Uhamiaji Zanzibar kwa kuwapelekea watoto misaada hiyo na kuwaomba mashirikiano
zaidi juu ya suala la kuwalea watoto hao.
Aidha Watoto
hao yatima wakiongozwa na mtoto Abdulrahman Aly Mussa walisoma dua maalum ya
kuwaombea wanawake hao ikiwa ni shukran kwao.
Kwa upande wa Zanzibar Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wanawake duniani ni ‘’Badili fikra: imarisha ushiriki wa wanawake katika maamuzi kwa maendeleo endelevu’’.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Vifaa mbali mbali vikitolewa na uhamiaji Zanzibar |
(Maafisa Uhamiaji Zanzibar wakishiriki kufanya usafi) |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Zanzibar) |
08 Machi 2021
Uhamiaji Iringa Yaendelea kutekeleza Maelekezo ya CGI Dkt. Anna Makakala
Ofisi ya Uhamiaji
Mkoa wa Iringa mapema wiki hii imeendelea kutekeleza maelekezo ya Kamishina
Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala kwa kutoa elimu ya Ki-uhamiaji kwa
kushirikiana na vyombo mbalimbali ya habari
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACI Agnes Luziga ameeleza kwamba Mkoa huo sasa umejiwekea mpango mkakati wa kuendelea kutoa elimu kwa umma mara kwa mara katika masuala mbalimbali ya Ki-uhamiaji
Kupitia 96.7 Radio Furaha Fm iliyopo Iringa mjini, wananchi wameweza kupata elimu ya aina za pasipoti na hati za kusafiria, ambapo Konstebo wa Uhamiaji Richard Nzagi pamoja na Konstebo Mariam Simba kutoka kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa wameelezea kwa kina vigezo vya kupata hati hizo za kusafiria ambazo ni pasipoti ya kawaida (Ordinary Passport), pasipoti ya utumishi(Service Passport), pasipoti ya kidiplomasia (Diplomatic Passport), hati ya utambulisho, hati ya kusafiria ya dharula na hati ya kusafiria ya mkataba wa Geneva.
Aidha wameeleza pia dhana ya Uhamiaji Mtandao ambapo ni muunganiko wa mifumo mbalimbali ya ki-uhamiaji ambayo imesanifiwa kufanya kazi kwa pamoja na kutoa taarifa kwa watumiaji na wadau wa huduma za ki-uhamiaji, huduma hizo ni e-Visa, e-Resident Permit, e-Passport, na e-Border Management.
Mbali na hayo walitoa pia elimu ya masuala ya uhamiaji haramu na madhara yake kwa ulinzi na usalama wa nchi yetu sanjari na kusisitiza kwamba suala la la ulinzi na usalama wa nchi ni jukumu la kila mtanzania hasa mzalendo.
#Zuia uhamiaji haramu.
HABARI PICHA NA MATUKIO
![]() |
Konstebo wa Uhamiaji Richard Nzagi pamoja na Konstebo Mariam Simba kutoka kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa wakitoa elimu kwa umma kwa njia ya redio mkoani Iringa |
![]() |
(Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa) |
05 Machi 2021
Uhamiaji Zanzibar yatoa mafunzo ya E-visa kwa wadau wa utalii na kampuni za usafirishaji
Zanzibar
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu ameongoza semina ya viza za kielektroniki kwa wadau mbali mbali wa utalii na kampuni za usafirishaji (ground handler) mapema mwaka huu katika ukumbi wa mkutano wa Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar.
Katika mkutano huo amewashajihisha wadau juu ya matumizi ya e-visa, badala ya kuomba visa wakati mgeni akiingia nchini (visa on arrival) ambayo inaombwa wakati mgeni anapowasili kupitia vituo vya kuingilia nchini ambapo imekuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuleta usumbufu kwa wageni, kwani hulazimika kujaza fomu ya maombi ya viza baadae kuwasilisha katika kaunta za Uhamiaji, kufanyiwa mahojiano, kupatiwa control namba kwa ajili ya malipo, kwenda benki kufanya malipo na kurudi tena katika kaunta za Uhamiaji kwa kupata ruhusa husika ya kuingia nchini.
Ni utaratibu wa kisheria na kifedha lakini hata hivyo umeonekana kuleta usumbufu kidogo kwa wageni wanaoingia hapa nchini.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha TEHAMA
Uhamiaji Zanzibar Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Muhsin Ali Masheko amezidi
kuwahamasisha wageni kuomba viza kwenye mtandao badala ya kuomba wakati wa kuingia nchini, sanjari na kuwaelezea athari za kuomba viza wakati wa kuwasili
nchini, pia ameeleza kuhusu pasipoti za kikimbizi na kuwataka wadau hao kuitambua pasipoti hiyo ya kikimbizi (convention
passport) ambayo hutumiwa na wageni wasiokuwa raia halisi wa nchi husika.
Aidha, mkuu huyo wa kitengo cha TEHAMA ameongeza kuwashajihisha wageni kujaza fomu za kuingilia nchini (TIF. 10) wakiwa nyumbani kabla ya kuingia nchini inayopatikana baada ya ombi kukubaliwa badala ya kusubiri kujaza kwenye ndege au wakiwa vituoni wanapoingia kwa ajili ya kupunguza muda wa kukaa katika kaunta za kupokelea wageni.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu akiongoza semina ya viza za kielektroniki kwa wadau mbali mbali wa utalii na kampuni za usafirishaji (ground handler) |
Wadau mbali mbali wa utalii na kampuni za usafirishaji wakifuatilia kwa makini semina ya viza za kielektroniki iliyotolewa na Idara ya Uhamiaji Zanzibar |
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Uhamiaji Zanzibar Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Muhsin Ali Masheko akitoa ufafanuzi juu ya huduma za e-Visa |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Zanzibar) |
04 Machi 2021
Balozi za Heshima zafurahishwa na Utoaji wa Huduma za Uhamiaji Zanzibar
Uhamiaji Zanzibar
Balozi za heshima Zanzibar kutoka Brazil, Ufaransa, Italy, Sweden, Spain, German, Uengereza na Canada zikiongozwa na Balozi wa heshima kutoka nchini Brazil Bw. Abdulsamad Abdulrahim wamesema kwamba wanafurahishwa na utoaji wa huduma za Ki-uhamiaji wakati wa kuingia na kutoka Zanzibar.
Hayo yamesema mapema leo katika Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar kwenye kikao kilichomshirikisha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar pamoja na balozi hizo za heshima.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu amezishauri Balozi za heshima zilizopo Zanzibar kuwashauri raia wao kuomba viza za kielektroniki pale wanapotaka kuingia nchini.
Aidha ameeleza kwamba Idara ya Uhamiaji imeanzisha viza za kielektroniki ambapo mgeni anaweza kuomba, kulipa na kupatiwa viza akiwa nje ya nchi jambo linalorahisisha kumhudumia mgeni kwa haraka zaidi wakati wa kuingia nchini.
“Mgeni anaeingia nchini kwa kuomba viza katika vituo vya kuingia hulazimika kufanyiwa mahojiano na Afisa Uhamiaji, kupatiwa namba ya malipo (control number) pamoja na kulazimika kufanya malipo katika kaunta za benki ya watu wa Zanzibar au CRDB zilizopo katika uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA)” alisema Kamishna Sururu.
Kwa upande wao balozi za heshima walisema Maafisa Uhamiaji wanatumia taaluma, uzoefu na bidii ya hali ya juu katika kutoa huduma kwa ufanisi, Balozi hizo zilielezea kufurahishwa na mfumo wa viza za kielektroniki ambapo sasa raia wao wanaomba na kupatiwa viza kwa njia ya mtandao hali inayorahisisha mgeni kuingia hapa nchini bila ya kupoteza muda.
Mabalozi hao wa heshima waliohidi kufanya kazi kwa pamoja na Idara ya Uhamiaji na waliahidi kuwatangazia raia wao kuomba viza ya kielektroniki.
Pamoja na kazi zao za kibalozi walifahamisha kuwa wanafanya jitihada za kuimarisha biashara hasa katika sekta ya utalii Zanzibar
Pia walifurahishwa na maamuzi ya Idara ya Uhamiaji katika kuongeza viza muda katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa covid 19, ambapo wageni ambao walishindwa kurejea nchini kwao kutokana na janga hilo lililoikumba dunia waliongezwa mwezi mmoja kuishi hapa nchini bila ya malipo.
Wameiomba Idara ya Uhamiaji kuangalia uwezekano wa kuanzisha utaratibu utakaowezesha wageni kupatiwa nyaraka zitakazowawezesha kurejea nchini kwao endapo watapoteza pasipoti zao wakiwa Zanzibar.
Kwa sasa mgeni anaepoteza pasipoti akiwa Zanzibar anatakiwa kwenda katika Afisi za Kibalozi za nchi zao zilizopo Dar-Es-Salaam, jambo ambalo linaonekana kuleta usumbufu hasa kwa wageni ambao safari zao zinakua siku za mwisho wa wiki au mapumziko.
Uhamiaji Kigoma yakamata Wahamiaji Haramu zaidi ya 70
Kigoma, Tanzania
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kigoma imewakamata wahamiaji haramu 73, ambapo 56 wamethibitika kuwa wahamiaji haramu na 17 uchunguzi wa uraia wao unaendelea na wote hawa wanashikiliwa kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mapema wiki hii Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji (ACI) Augustino Matheo amesema Idaa ya uhamiaji mkoa imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu hao kutokana na kufanyika doria na misako mbalimbali iliyofanyika tarehe 03 Machi 2021.
ACI Matheo amefafanua zaidi kwamba waliokamatwa nia raia 51 wa nchi jirani ya Burundi, raia wa Kongo DRC 04, raia wa Rwanda 01 na Wanaodai ni raia wa Tanzania17 ambapo uchunguzi unaendelea ili kubaini uraia wao.
“Wahamiaji haramu hawa wamekamatwa katika mwalo wa ziwa Tanganyika eneo la Kibirizi mkoani Kigoma, Katika maelezo yao tumegundua walikuwa wanajishughulisha na uvuvi” alisema ACI Matheo
Aidha ametoa tahadhari kwa mwananchi yeyote atakayekutwa amewahifadhi wahamiaji haramu katika nyumba yake au akiwa anawasafirisha kwenye gari (chombo cha usafiri) atachukuliwa hatua kali za kisheria zikiwemo kushitakiwa mahakamani, nyumba au chombo alichokua anakitumia kusafirishia au kuwahifadhia wahamiaji haramu vinaweza kutaifishwa na Serikali kwa mujibu wa sheria.
Ameongeza kwamba tayari hatua zimechukuliwa mara baada ya kukamilisha taratibu zote watafikishwa mahakamani ka kosa la kuingia nchini kinyume na sheria za nchi.
“Wale wote wanaoingia nchini kupitia vipenyo visivyo rasmi (Panya Roots) tutawakamata wote, vilevile tunawaomba wananchi watupe ushirikiano pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili tuwabaini wahamiaji haramu na mtandao wao” alisema
Onyo limetolewa kwa Mkoa wa Kigoma kwamba Mkoa huo sio kichaka wala njia au maficho ya wahamiaji haramu kupitia kwenda sehemu zingine za nchi, kwani Idara imejipanga kidete kuwezesha na kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu kupitia utekelezaji wa sheria na kanuni zilizopo ili kulinda usalama wa Taifa na kukuza maendeleo ya kiuchumi.
HABARI PICHA NA MATUKIO
![]() |
Baadhi ya wahamiaji haramu waliokamatwa Mkoani Kigoma kwa kuingia chini kinyume na sheria |
![]() |
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji (ACI) Augustino Matheo akitoa taarifa kwa umma ofsini kwake |
![]() |
(Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Kigoma) |
01 Machi 2021
Uhamiaji Tanzania Yatwaa Tuzo Mbili kwa Mpigo #Tanzania Digital Awards 2020
Dar es salaam
Idara ya Uhamiaji Tanzania imeibuka na Ushindi wa tuzo mbili za mwaka 2020 zilizoandaliwa na kampuni ya Serengeti Byates maarufu kama Tanzania Digital Awards (TDA) 2020 baada ya kupata kura nyingi kutoka wadau mbalimbali na watumiaji wa huduma za Ki-uhamiaji na kushindanishwa na taasisi mbalimbali katika vipengele vya Digital Innovation of the year na Best Government Agency on Digital ambapo Uhamiaji ilishinda tuzo zote hizo.
Akipokea tuzo hizo katika ofisi za Uhamiaji Kurasini Dar es salaam Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala ameishukuru kampuni hiyo kwa kuandaa mashindano hayo kwani yamesaidia kujua namna gani huduma za ki-uhamiaji zinawafikia watanzania na raia wa kigeni kwa viwango bora vya kitaifa na kimataifa.
Aidha Dkt. Makakala amewashukuru wale wote walioshiriki kuipigia kura Idara ya uhamiaji katika vipengele vyote na hatimae kupata ushindi huo mkubwa ambao unabaki kuwa alama kubwa na kuwaahidi kuongeza uhodari na weledi wa hali ya juu ili kuongeza ufanisi zaidi katika kutoa huduma za Ki- Uhamiaji kwa faida ya kizazi cha sasa na baaae
Akikabidhi tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Byates Kennedy Mmali amepongeza Idara ya Uhamiaji kwa Ushindi huo kwani wamekuwa wabunifu zaidi kiasi cha kuzishinda taasisi nyingine za serikali.
Mashindano hayo ya Serengeti Byates kwa mwaka 2020 yalihusisha taasisi zaidi ya 50 za serikali na hatimaye uhamiaji kuibuka kidedea.
Hafla hiyo ya kukabidhi tuzo pia ilihudhuliwa na Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Pasipoti na Uraia (CI) Gerald Kihinga, Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Udhibiti wa Mipaka (CI) Samweli Mahirane, Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Vibali vya Ukaazi Visa na Pasi (CI) Mary Palmer ndc na Pasi pamoja na Maafisa na Askari wa Uhamiaji.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akipokea tuzo za Tanzania Digital Awards 2020 kutoa kwa waandaaji kampuni ya Serengeti Byates |