Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

10 Februari 2021

Uhamiaji Zanzibar yashiriki maandamano ya amani ya siku ya sheria


Idara ya Uhamiaji Zanzibar mapema wiki hii imeshiriki maandamano ya amani ya  siku ya sheria Zanzibar  yaliyoanzia Vuga  na kumalizia katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.

Maandamano hayo yalipokelewa na mgeni rasmi wa maadhimisho hayo, Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman.

Katika kufanikisha maadhimisho hayo michezo mbali mbali ilioneshwa ikiwa ni pamoja na mchezo wa kuvuta kamba na mazoezi mbali mbali kwa washiriki wote.

Walioshiriki uvutaji kamba ni majaji na wanasheria kutoka afisi ya Jaji Mkuu, afisi ya bandari, KMKM na kikundi cha kitambi noma ambapo washindi walitangazwa na kupongezwa na mgeni rasmi,  Kmkm na kitambi noma ndio walikua washindi wa mchezo huo dhidi ya wanasheria na Bandari.

Aidha mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar aliwashukuru waandaaji wote pamoja na afisi ya Jaji mkuu kwa kufanikisha zoezi hilo, vile vile amewataka washiriki wote wawe na tabia ya kufanya mazoezi kila siku kitu ambacho kitawajengea afya imara.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kuvuta Kamba

Mazoezi yakiendelea













(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Afisi kuu  Zanzibar)

09 Februari 2021

KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI AFANYA ZIARA YA KIKAZI JIJINI DAR ES SALAAM

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala mnamo siku ya Jumatatu Februari 8, 2020 amefanya ziara ya kikazi ya siku moja jijini Dar es salaam. Katika ziara hiyo, Dkt. Makakala amemtembelea Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Aboubakar Kunenge na kuongea nae kuhusu masuala ya uhamiaji katika mkoa huo.

Kamishna Jenerali pia alitembelea ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ubungo na kuongea na Mkuu wa Wilaya Mh. Kisare Makori, ambapo pia alifanya ukaguzi wa ofisi ya Uhamiaji (W) Ubungo na kuzungumza na Askari pamoja na Watumishi kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili. Baada ya mazungumzo hayo, Kamishna Jenerali alikwenda kukagua kituo kipya cha Uhamiaji ndani ya stendi mpya ya Mabasi Ubungo.

Ziara hiyo ya Siku moja jijini Dar es salaam ilifikia tamati kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji  kukagua kiwanda cha uchapishaji na ushonaji cha Idara ya uhamiaji kilichopo kijichi Jijini Dar es salaam. Katika ukaguzi huu alisisitiza watendaji waongeze kasi na weledi ili kufikia malengo yanayotarajiwa.


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akisikiliza maelezo ya namna ya shughuli za ushonaji zinavyofanyika katika Kiwanda cha Ushonaji cha Uhamiaji, Kijichi Dar es salaam



Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Abubakar Kunenge mara baada ya mazungumzo ya kikazi katika ofisi za mkuu huyo wa mkoa.









05 Februari 2021

IDARA ya Uhamiaji yapongezwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuendelea kutekeleza vyema majukumu yake.

Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa pongezi hizo wakati alipokuwa na mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI)  Dkt. Anna Peter Makakala, aliyefika Ikulu Jijini Zanzibar, kwa ajili ya kujitambulisha.

Katika maelezo yake, Rais Dkt
. Mwinyi alitoa pongezi kwa Idara hiyo ya Uhamiaji kwa kuanza kuzifanyia kazi changamoto zilizokuwepo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani karume hatua ambayo itapunguza foleni kwa wasafiri wakiwemo wageni ambao lengo ni warudi tena kuja kuitembelea Zanzibar.

Alisema kuwa changamoto ya foleni ilikuwa ikiwasumbua sana wasafiri wakiwemo wageni hasa ikizingatiwa kwamba uwanja wa ndege huo ni lango la watalii kutoka nje ya nchi hivyo, kupatikana na ufumbuzi huo kutaweza kusaidia.

Aliongeza kuwa juhudi za makusudi zitachukuliwa katika kuhakikisha jengo jipya la uwanja wa ndege litakapoanza kazi changamoto kama hizo hazijitokezi.

Alipongeza kwa kuongeza kwa madawati na kufikia 28 ambazo zimeanza kusaidia na kupunguza foleni katika uwanja wa ndege huo hasa pale wakati zinazotua ndege nyingi kutoka nje kwa wakati mmoja.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kwa kuzifanyia kazi changamoto hizo na kupelekea kuongeza madawati katika uwanja huo wa ndege wa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi alitoa ushauri kwa Idara hiyo ya Uhamiaji kuwa ni vyema kuhakikisha kila mgeni anaekuja awe ameshapata VISA yake ili kuondosha kukaa foleni muda mrefu katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.

Pamoja na hayo, Rais Dk. Mwinyi alisisitiza kwamba kwa vile uchumi wa Zanzibar unaitegemea kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii hivyo, ni vyema kwa kila mdau kwa upande wake akahakikisha anatoa mchango wake katika kufanikisha jambo hilo.

Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuipongeza Idara hiyo kwa kazi kubwa iliyoifanya ya kushiriki katika kuleta amani nchini katika wakati wa uchaguzi hatua ambayo bado wanaendelea nayo.

Aidha, alipokea pongezi za kushinda nafasi ya kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu uliopita wa Oktoba 2020.

Mapema Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala alimpongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kushinda kwa kishindo katika uchaguzi uliopoita wa Oktoba 2020 na kuwa Rais wa Zanzibar Awamu ya Nane.

Dkt. Makakala alitoa shukurani zake yeye pamoja na Idara yake ya Uhamiaji na kupongeza mashirikaino yaliopo kati yake na Kamishna wa Uhamiaji wa Zanzibar Johari Masoud Sururu hatua ambayo alisema inazidi kuiimarisha Idara hiyo.

Alisema kuwa kazi za Idara hiyo zitaendelea kuimarishwa kwa weledi na kutoa ushirikiano sambamba na kupokea maelezo kwa Rais Dkt. Mwinyi ili kuimarisha vyema kazi za Idara hiyo.

Alisema kuwa Idara hiyo imeimarisha mifumo ya utoaji wa huduma na kuimarisha mfumo wa Uhamiaji Mtandao ambapo tayari wameshaanza kutoa pasi za kusafiria za elektroniki ambapo pasi hiyo iliweza kushinda kimataifa.

Aidha, alisema kuwa Idara hiyo inatoa VIZA kwenye mitandao, vibali vya ukaazi pamoja na udhibiti wa mipaka ambapo hatua hiyo imeweza kuimarisha mapato kwa kiasi kikubwa.

Alisema kuwa tokea mifumo hiyo ianze mapato yameweza kuongezeka ambapo mnamo mwaka 2015 kabla ya kutumika kwa njia ya mifumo ya mtandao Idara hiyo ilikusanya Bilioni 10 kwa upande wa Zanzibar na mwaka 2016 ilikusanya Bilioni 17.7  ambapo mwaka 2017 ilikusanya Bilioni 23.

Aliendelea kueleza kwamba kuanzia mwaka 2018 walipoanza kutumia mfumo mtandao Idara hiyo iliweza kukusanya bilioni 28.9 na mwaka 2019 ilikusanya bilioni 31 ambapo mwaka 2020 ilikusanya bilioni 33 licha ya kuwepo changamoto kadha ikiwemo ugonjwa wa Covid 19.

Pamoja na hayo,CGI Dkt. Makakala alisema kuwa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar kumekuwa na changamoto ya kupambana katika kutoa huduma bora kwa watalii na wananchi kutokana na ndege kutua kwa wakati mmoja sambamba na uwanja mmoja kutumia ndege za ndani na nje.

Alisema kuwa  licha ya hali hiyo kutokana na kuimarisha mifumo wameweza kuongeza madawati na kufikia 28 na kuweza kutoa huduma ambapo ndege yenye abiria 400 wanaweza kuhudumia kwa saa moja.

Pia, kutokana na uhaba wa wafanyakazi wa Idara hiyo imeweza kuongeza wafanyakazi kutoka 68 na kufikia 113 huku wakichukua juhudi ya kuomba Mamlaka ya uwanja wa ndege kupeana muda jambo ambalo limekubalika jambo ambalo litaleta faraja.

Kamishna  Jenerali huyo alieleza matarajio yake katika jengo jipya la uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume (Terminal III)  linalotarajiwa kuanza  kazi hivi karibuni.

Alieleza juhudi zilizochukuliwa kiwanjani hapo ambapo abiria hivi sasa hana haja ya kupita katika sehemu nne za madawati kama ilivyokuwa hapo awali huku akieleza kwamba tayari wameshapata vifaa ambapo wageni wanaweza kulipa hapo hapo uwanjani iwapo watakuwa na kadi za benki.

Alisema kuwa mbali ya kusimamia ulinzi na usalama Idara hiyo imehakikisha inachangia mapato na uchumi wa nchi sambamba na kuendelea na kazi zake za kufanya misako mbali mbali nchi nzima ili kuhakikisha wahamiaji haramu wanaoingia nchini bila ya kufuata taratibu wanachukuliwa hatua stahili.

 HABARI PICHA NA MATUKIO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt.Anna Peter Makakala (kulia kwa Rais) alipofika Ikulu ya Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha akiwa na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu

 

(Picha kwa hisani ya Ikulu Zanzibar)


28 Januari 2021

UHAMIAJI Tanzania Yapokea Pikipiki Kutoka Shirika la Kimataifa la Uhamiaji

Dodoma, Tanzania

Idara ya Uhamiaji Tanzania mapema leo hii imepokea pikipiki 04 kutoka shirika la kimataifa la Uhamiaji ikiwa ni mchango mojawapo wa miradi yenye malengo ya kuongeza uwezo wa vitengo vya doria mpakani kwenye idara na kusimamia uhamiaji haramu. 

Akipokea pikipiki hizo katika ofisi ya makao makuu ya Uhamiaji Dodoma, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala amelishukuru shirika hilo kwa mchango wake mkubwa katika kusaidia Idara ya uhamiaji kutekeleza majukumu yake hasa katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu nchini.

CGI Dkt. Makakala amesema kwamba pikipiki hizo zimefika wakati muafaka na zitaenda kusaidia zaidi mipakani ili kuimarisha doria na misako kwani Uhamiaji holela unapaswa kupingwa, kwa sababu ni hatari na mbaya kwa usalama wa taifa.

Aidha ameliomba shirika hilo kuendelea kushirikiana zaidi katika shughuli zake zingine zikiwemo za kusaidia vifaa muhimu vinavyohitajika katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma kichakamiba iliyopo Wilayani Mkinga Mkoani Tanga.

Kwa upande wake Katibu Mkaazi wa IOM, Dr Qasim Sufi akitoa maelezo ya awali ya mchango wa pikipiki katika Idara ya Huduma za Uhamiaji alisema amefurahi sana kushiriki na kuiwakilisha IOM katika shughuli hiyo muhimu ya kukabidhi pikipiki kwa Idara ya Uhamiaji.

“Wengi wenu mtakuwa mnafahamu kwamba, mwaka jana Julai 2020 Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM), Shirika la Uhamaji la Umoja wa Mataifa (UN) lilitoa pikipiki tano za Honda XL125 na leo tarehe 28 Januari 2021, linafuraha kutoa Honda 4 zaidi aina ya XL125 katika Idara ya Huduma za Uhamiaji” alisema Dr Qasim Sufi

Mchango huu muhimu (wenye thamani ya dola za kimarekani elfu ishirini na tano 25,000) unatolewa na IOM chini ya Mradi wa Uhamaji wa ukanda wa Afrika – ikiwa ni awamu ya 10 katika Ukanda wa Mashariki na Pembe ya Afrika ulioyofadhiliwa na Idara ya Serikali Ofisi ya watu, Wakimbizi na Uhamiaji (BPRM) wa Nchini Marekani (USA)

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akipokea pikipiki kutoka kwa Katibu Mkaazi wa IOM, Dr Qasim Sufi katika ofisi za makao makuu ya Uhamiaji Dodoma

Pikipiki zilizokabidhiwa 





Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akisaini hati ya makabidhiano ya pikipiki katika ofisi za makao makuu ya Uhamiaji Dodoma

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala na Katibu Mkaazi wa IOM, Dr Qasim Sufi wakionesha hati za makabidhiano ya pikipiki 04 katika ofisi za makao makuu ya Uhamiaji Dodoma




(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

26 Januari 2021

UHAMIAJI IRINGA YASHIRIKI MAONESHO YA UWEKEZAJI

 Iringa, Tanzania

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa imeshiriki maonesho ya mwongozo wa uwekezaji mkoa wa Iringa, Maonesho hayo yalifunguliwa tarehe 23 January 2021 na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) katika viwanja vya maonesho vya chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE).

Katika maonesho hayo yaliyodumu kwa siku mbili huduma mbalimbali za ki-uhamiaji zilitolewa kama vile ukaguzi na upitishaji wa fomu za vitambulisho vya taifa, elimu ya uraia, elimu juu ya uhamiaji haramu na madhara yake kwa jamii na taifa kwa ujumla sanjari na  kupokea maombi ya passipoti ya kielektroniki n.k.

Maonesho hayo yalijumuisha taasisi za uuma na binafsi zinazotoa huduma katika Mkoa wa Iringa.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Elimu ikitolewa





(Picha zote na kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa)