MSHINDI WA SHINDANO BENKI YA NBC AKABIDHIWA PASIPOTI
Kamaishna Msaidizi wa uhamiaji na Mkuu wa kitengo cha pasipoti Dorah Luoga akikabidhi pasipoti kwa mshindi wa shindano la kuweka akiba katika Benki ya NBC Bi. Rebeka Joshua Marwa katika Ofisi ndogo ya Uhamiaji Makao Makuu Dar es salaam.
Makabidhiano hayo yalihudhuriwa na maafisa toka benki ya NBC Pamoja na Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu Mwandamizi Alhaj Ally Mtanda. Kwa ushindi huo Bi. Rebeka Joshua Marwa anatarajia kwenda nchini Shelisheli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni