Dar es salaam
Akifanya Kikao na Watumishi kituoni hapo Dkt.Makakala amewataka watumishi wote wanaofanya kazi katika kituo hicho kufanya kazi kwa nidhamu, utii, uhodari, na weledi na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ikiwemo kutojihusisha na masuala ya rushwa.
Aidha ameapa kutowavumilia maafisa askari na watumishi wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa na kwamba atawachukulia hatua kali za kinidhamu ikiwemo kuwafuta kazi na kuwafikisha mahakamani.
Sanjari na hilo amesisitiza pia kuongeza juhudi za ukusanyaji maduhuli ya serikali ili kuongeza pato la taifa na kuchochea maendeleo kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae.
Ili kuongeza ufanisi zaidi katika utekelezaji wa majukumu ya ulinzi na usalama wa nchi kupitia mipaka na njia zote za kuingilia na kutokea nchini, Dkt. Makakala amewataka maafisa na askari wote kushirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha nchi inakuwa salama.
Ziara ya Kamishina Jenerali ni muendelezo wa ziara za mara kwa mara katika kukagua shughuli za utendaji kazi ili kuhakikisha idara inafikia malengo yake mahususi ya utendaji kwa kutoa huduma za uhamiaji zenye kukudhi viwango vya kitaifa na kimataifa.
HABARI NA MATUKIO
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala Akitoa Maelekezo kwa Maofisa, Askari na watumishi wa Uhamiaji katika Kituo cha Uhamiaji cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNIA) Jijini Dar es salaam.
Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Makao Makuu ya Uhamiaji |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni