Wadau wa huduma za Uhamiaji waliohudhuria mkutano huo katika Ukumbi wa Mount Meru Hotel jijini Arusha. |
Mkutano wa Idara ya Uhamiaji na Wadau wa Huduma za
Uhamiaji mkoa wa Arusha umefanyika leo tarehe 2 Disemba 2019 katika Ukumbi wa
Mount Meru Hotel jijini Arusha. Mgeni rasmi wa mkutano huo alikuwa Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo aliyewakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Bi.
Thresia Mahongo.
Lengo
la mkutano huo ni kuwakutanisha Wadau wa huduma za Uhamiaji Mkoani Arusha na kuwajengea
uelewa juu ya masuala mbalimbali ya Kiuhamiaji, hususani huduma za
Kielektroniki; pamoja na kupokea maoni kutoka kwa wadau hao ili kutatua changamoto
mbalimbali na kuboresha huduma za Uhamiaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni