Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Dkt. Anna Peter Makakala jana tarehe 26 Disemba 2019 ameongoza waombolezaji
waliohudhuria ibada ya kumuaga Kamishna Msaidizi Mwandamizi mstaafu Sylvester
Peter Ngonyani aliyefariki usiku wa kuamkia tarehe 25 Disemba 2019.
Ibada hiyo ilifanyika nyumbani
kwa marehemu Toangoma Kigamboni, ambapo mbali na kuhudhuriwa na Kamishna
Jenerali, Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha, Maafisa Waandamizi wa
Uhamiaji, Maafisa, askari na watumishi wengine wa Uhamiaji walihudhuria katika ibada
hiyo.
Marehemu Sylvester Peter
Ngonyani aliajiriwa Idara ya Uhamiaji mwaka 1990
Marehemu
alizaliwa tarehe 09 Disemba 1964 katika Kijiji cha Ngoheranga
wilayani Malinyi Mkoa wa Morogoro, alisoma shule ya msingi Ngoheranga baadaye
Kibasila na Shycom kwa elimu ya sekondari. Pia elimu ya juu aliipata Chuo Kikuu
cha Mzumbe. Aliajiriwa na Idara ya Uhamiaji Mwaka 1990, na kushika nyadhifa
mbalimbali mpaka anastaafu mwishoni mwa mwaka huu marehemu Ngonyani alikuwa Mkuu
wa Kitengo cha Anuai za Jamii Makao Makuu ya Uhamiaji. Marehemu ameacha Watoto
watano na wajukuu wawili. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni