Matangazo

📢 IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA — KARIBU KWENYE BLOG RASMI   ✦   📰 UHAMIAJI HABARI BLOGU — TUNAKULETEA MATUKIO KILA SIKU   ✦   📲 FUATA IDARA YETU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII   ✦   ✉️ WASILIANA NASI: info@immigration.go.tz   ✦   ☎️ +255-22-2850575/6

05 Machi 2020

Uhamiaji na Airtel Wazindua Huduma za Malipo ya Ada ya Pasipoti kwa njia ya Airtel Money


Dar es salaam, Tanzania
Idara ya Uhamiaji Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya mawasiliano ya Airtel mapema leo hii tarehe 5 Februari 2020 tumezindua huduma ya malipo ya ada za pasipoti kwa njia ya Airtel Money ili kuongeza wigo wa malipo ya huduma za pasipoti.

Mgeni rasmi wa Uzinduzi huo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Mohamed Awesu ambae pia ndie Mfawidhi Mkuu wa TEHAMA Katika Jeshi la Uhamiaji Tanzania amesema Matumizi ya huduma hii yatamrahisishia mwombaji wa pasipoti kufanya malipo kutoka mahali popote alipo.

“Ili kutumia huduma hii mteja anatakiwa kutembelea tovuti ya Idara ya Uhamiaji (www.immigration.go.tz), atajaza fomu yake na baada ya kukamilisha kujaza atapatiwa Namba ya Kumbukumbu ya malipo (Control Number) ambayo ndiyo ataitumia kufanya malipo kwa njia hiyo ya Airtel Money. Baada ya hapo ataiprint na kisha kuiwasilisha fomu hiyo katika Ofisi ya Uhamiaji kwa taratibu zinazofuata” alisema.

Hatua ya kutumia huduma hii ya Airtel Money ni utekelezaji wa sera ya Serikali ya kwa taasisi zake zote kufanya malipo ya huduma mbalimbali kupitia Mfumo wa Serikali wa malipo kwa njia ya Mtandao GePG.

Mfumo huo umerahishisha sana malipo na umekuja na faida nyingi kama vile kurahisisha malipo, kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu, kupunguza upotevu wa mapato ya Serikali, kuondoa mianya ya rushwa pamoja na kuongeza mapato ya serikali.

Aidha SACI Awesu ameipongeza Kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuweza kuungana na Huduma za Uhamiaji kama ilivyo kwa mitandao mingine ya mawasilano hapa nchini ili kuwawezesha Watanzania kufanya malipo ya pasi za kusafiria kwa kutumia huduma ya “Airtel Money”, hatua hii inaendelea kurahisisha na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma ya Pasipoti.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania Bw. Isack Nchunda, amemshukuru Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala kwa  ushirikiano mkubwa aliouonesha wakati wote wa mchakato wa kuelekea tukio hili la ufunguzi wa huduma hii ili kuwarahisihia wananchi kupata huduma ya pasipoti kwa urahisi na kufanya malipo sehemu yoyote ile.

Bwana Nchunda aliongeza kuwa mwombaji anaweza kulipa ada yake ya maombi ya  pasipoti baada ya kupewa kumbukumbu ya malipo (Control Number) ambapo unapiga *150*60# Unachagua kufanya malipo Namba 5, Kisha unachagua malipo ya serikali, halafu unaingiza namba ya kumbukukumbu ya malipo unaweka kiasi kama ni ada ya fomu ya Pasipoti ambayo gharama yake ni Tsh 20,000tu na ada ya Pasipoti baada ya kuprinti fomu zikishakaguliwa na Maafisa Uhamiaji Unamalizia Tsh.130,000 tu ambayo huleta gharama ya pasipoti kwa Tsh. 150,000tu.

Sanjari na hilo unamalizia kwa kuingiza namba zako za siri na kisha unathibitisha malipo yako na ndani ya sekunde 10 mpaka 15 unapata ujumbe wa malipo yako kupokelewa.

Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Money ni Kampuni inayomilikiwa na serikali kwa asilimia 49% ndio maana inarahisisha maisha kwa kushirikiana na Uhamiaji, kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora kupitia Airtel Money kwa haraka na uhakika zaidi.

Mfumo wa Uhamiaji Mtandao ulizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli tarehe 31 Januari, 2018. Tangu wakati huo, fomu za maombi ya Pasipoti zimekuwa zikijazwa kwa njia ya mtandao, Hivyo Uhamiaji Tanzania inatoa wito kwa wananchi kuendelea kutumia huduma hii ya Airtel Money katika kufanya malipo yao ya ada za pasipoti kwani ni salama na rahisi kutumia.

 HABARI PICHA NA MATUKIO
Mgeni rasmi wa Uzinduzi huo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Mohamed Awesu (katikati) ambae pia ndie Mfawidhi Mkuu wa TEHAMA Katika Jeshi la Uhamiaji Tanzania akipokea alama ambayo ni Ishara ya Uzinduzi wa  malipo ya Ada ya Pasipoti kwa njia ya AirtelMoney




Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Dorah Luoga (katikati) ambae pia ndie Mdhibiti wa Pasipoti Katika Jeshi la Uhamiaji Tanzania ajitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania Bw. Isack Nchunda Pasipo kupeana mikono ikiwa ni Utekelezaji wa Ushauri wa Waziri wa Afya, hapa ni katika uzinduzi wa  malipo ya Ada ya Pasipoti kwa njia ya AirtelMoney katika Ofisi Ndogo za Uhamiaji Makao Makuu Kurasini Dar es salaam
Huduma zikiendelea kutolewa kwa wateja kujua namna ya kulipia pasipoti kwa njia ya Airtel Money




Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania Bw. Isack Nchunda akitoa maelezo mafupi ya namna ya kufanya malipo ya ada ya pasipoti kwa njia ya Airtel Money

Afisa Uhusiano Mrakibu Msaidizi akiongoza itifaki katika tukio zima la Uzinduzi wa Huduma ya malipo ya ada ya Pasipoti kwa njia ya Airtel Money





Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Mohamed Awesu (kulia) ambae pia ndie Mfawidhi Mkuu wa TEHAMA Katika Jeshi la Uhamiaji Tanzania akitoa salamu ya kuagana na Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Dorah Luoga (kushoto) ambae pia ndie Mdhibiti wa Pasipoti Katika Jeshi la Uhamiaji Tanzania baada ya kumaliza tukio la uzinduzi wa malipo ya Ada ya Pasipoti kwa njia ya Airtel Money


Uhamiaji Tanzania Jazz Band nayo haikubaki Nyuma ilisindikiza Tukio hilo kwa kutoa Burudani kabambe kwa wateja walihudhuria tukio hilo

KATIBU MKUU ALIPOTEMBELEA MAKAO MAKUU YA UHAMIAJI DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Christopher Kadio akiingia katika ofisi za Makao makuu ya Uhamiaji jijini Dodoma alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi wa Idara hiyo leo tarehe 5 Machi 2020.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu WMNN Ndugu Christopher Kadio alipofanya ziara ya kikazi katika makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dodoma. 


Awali Katibu Mkuu Ndugu Kadio alifanya kikao cha ndani na Makamishna wa Uhamiaji katika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dodoma.



Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Makakala akimkaribisha Katibu Mkuu kuongea na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu jijini Dodoma

Baadhi ya Maafisa Uhamiaji wakifuatilia kwa karibu hotuba ya Katibu Mkuu
















Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Sururu akifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu WMNN leo taerehe 05 Machi 2020.

Katibu Mkuu WMNN Ndugu Kadio akiandika maoni ya mmoja wa wachangiaji alipokutana na watumishi wa Idara ya Uhamiaji jijini Dodoma.

Mtumishi wa Idara ya Uhamiaji Dereva Mwandamizi Beno Kereti akitoa maoni wakati wa kikao na Katibu Mkuu WMNN





Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar akitoa neno la shukrani kwa ujio wa Katibu Mkuu WMNN mara baada ya kuongea na Maafisa, Askari na Watumishi raia katika ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu jijini Dodoma.


04 Machi 2020

Dkt. Makakala awataka Maafisa Uhamiaji Mikoa Yote Nchini Kutoa Elimu ya Uhamiaji na Uraia kwa Wananchi


 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dtk. Anna Peter Makakala amewataka Maafisa Uhamiaji Mikoa wote nchini kujita zaidi katika kutoa Elimu ya Uhamiaji na Uraia kwa Watanzania. Hayo ameyasema leo Jumatano tarehe 4 Machi 2020 alipotembelea Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma kwa ziara ya Kikazi.



Akizungumza na Maafisa na Askari wa Uhamiaji, Dkt. Makakala amewata Maafisa Uhamiaji Mikoa wote nchini kuandaa programu maalum za Elimu ya Uraia kwa Umma kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi hususan katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.


"Nchi yetu Mwaka huu inafanya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani hivyo ni rai yangu kwa Maafisa Uhamiaji Mikoa kushirikiana vyema na Tume ya Uchaguzi kwa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi na kushughulikia changamoto za uraia zitakazo jitokeza wakati wa kipindi cha uchaguzi na kuhakikisha kuwa wanazipatia majibu kwa  wakati" amesema Dkt. Makakala.


Vilevile Dkt.  Makakala ametoa wito kwa Maafisa Uhamiaji Mikoa hao  kuhakikisha kuwa Wageni wote wanaoishi katika maeneo yao wanaishi kwa kufuata sheria.


Aidha, Maafisa Uhamiaji wote wametakiwa kuimairisha Doria na Misako ya Wahamiaji haramu kote nchini ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inabakia kuwa salama na Wahamiaji haramu hawanufaiki na rasilimali zetu.


Kwa Upande wake Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia Divisheni ya Vibali vya Ukaazi, Visa na Pasi, Mary Palmer (ndc) amewataka raia wa kigeni wote wanaoishi nchini kuhakikisha kuwa wana vibali vya Ukaazi.


Kamishna Palmer amesisitiza kuwa wageni wanaohitaji kuingia na kuishi nchini kwa madhumuni mbalimbali wanaweza kufanya maombi, kulipia na kupokea nakala za vibali vyao kwa njia ya mtandao.


Awali akitoa taarifa ya Utendaji kazi ya Mkoa, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Abdallah Katimba ameeleza kuwa Mkoa wa Dodoma umeimarisha Doria na Misako dhidi ya Wahamiaji haramu, na pia Mkoa umejipanga vyema kutoa Elimu ya Uraia kwa Watanzania.



Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akiongea na mmoja wa wateja wa huduma za Uhamiaji katika ofisi ya uhamiaji mkoa Dodoma.










Baadhi ya Askari na Maafisa wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji alipofanya ziara katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma.

Afisa Utumishi Mkuu Ndugu Mulegi Majogoro akiongeaa wakati wa kikao cha Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji alipozuru ofisi ya Mkoa jijini Dodoma leo tarehe 04 Machi 2020.


FULL VIDEO: Makala Maalumu ya Ziara ya Waziri Simbachawene Katika Jeshi ...

02 Machi 2020

Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara atoa Elimu ya Uhamiaji kwa Waalimu.


Na Mwandishi Wetu, Mtwara Tanzania

Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi James A. Mwanjotile amewaasa walimu wa Mkoa wa Mtwara kushirikiana na Idara ya Uhamiaji ndani ya mkoa huo katika kutoa taarifa za wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume cha sheria.

Ameyasema hayo katika mkutano wa uongozi wa baraza la chama cha walimu Mkoa wa Mtwara baada ya kualikwa na kutumia fursa hiyo kutoa elimu juu ya ushiriki wa wananchi katika kulinda usalama wa nchi  na mipaka yake.

Mkoa wa mtwara umepakana na nchi jirani ya msumbiji ambapo kumekuwa na matukio mbalimbali ya wahamiaji haramu kuingia  nchini kupitia njia zisizo rasmi katika vijiji mbalimbali vinavyopakana na nchi jirani ya Msumbiji na baade kuleta madhara ya uhalifu ndani ya Mkoa wa Mtwara.

"Napenda kutumia fursa hii kutoa wito  kwenu nyinyi  wajumbe wa baraza la waalimu Mkoa, na  wakaazi wa Mkoa huu ambao wengi wenu mnatoka maeneo ya mipakani tunaomba muweze kusaidia kutoa taarifa mbalimbali za wahamiaji haramu au pale mnapoona viashiria vyovyote vya watu msiowafahamu na mnashaka nao katika maeneo yenu tafadhali toeni taarifa mapema ili tuweze kuchukua hatua haraka iwezekanavyo, kwani jukumu la ulinzi wa nchi na Mipaka yake ni Jukumu letu sote”Alisema

Aidha amewasihi kuwa mabalozi wazuri kwa kuwaelimisha wanafunzi na wananchi wengine waishio maeneo mbalimbali ya Mkoa huo  kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa zozote za wahamiaji haramu na hata pale watakapoona ama kuhisi mtu yeyote ambae si raia wa Tanzania ameingia nchini kinyume na sheria basi waweze kuwasiliana nae kupitia namba zake za simu ya mkononi alizozitoa  au kuripoti katika ofisi yoyote ya Uhamiaji iliyopo karibu nae.

 HABARI PICHA NA MATUKIO 
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi James A. Mwanjotile akitoa Elimu ya Uhamiaji kwa Uongozi wa Baraza la Chama cha Walimu Mkoa wa Mtwara.
Baadhi ya viongozi wa Baraza la Chama cha Walimu Mkoa wa Mtwara wakimsikiliza kwa makini Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi James A. Mwanjotile 
(Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Mtwara)