Kamishna wa Uhamiaji (Pasipoti na Uraia) Gerald Kihinga (katikati) akiwa na Tuzo hio |
Pasipoti Mpya ya
Tanzania ya Kielektroni imetunikiwa Tuzo ya Pasipoti Bora katika Ukanda wa Ulaya,
Mashariki ya Kati na Afrika (Europe, Middle East and Africa - EMEA) kwa kukidhi
Viwango vya Ubora wa Kimataifa vinavyopendekezwa na Shirika la la Umoja wa
Mataifa linalosimamia Usafiri wa Anga (International Civil Aviation
Organisation - ICAO) kwa Mwaka 2019 katika Sherehe zilizofanyika Kisiwa cha
Malta siku ya Jumanne tarehe 26 Machi 2019.
Tuzo ambazo
huaandaliwa na kutolewa na Taasisi ya RECONNAISSANCE ambayo huzingatia ubora na
usalama wa Uchapishaji wa Nyaraka za Kielektroniki kama vile Vitambulisho vya Taifa,
fedha za noti na Pasipoti. Vipengele vinavyozingatiwa katika Tuzo hizi ni
pamoja na Usalama wa nyaraka, Usanifu, tekinolojia, na Utambulisho wa nchi.
Katika kipengele cha
utambulisho wa nchi yetu (National Identity), Pasipoti hii imesanifiwa kwa
kuzingatia utamaduni wa Kitanzania na maliasili tulizonazo ambazo ni fahari ya
nchi yetu. Michoro iliyopo katika Pasipoti hiyo ni pamoja Wanyama, majengo ya
kihistoria, Matukio ya Kitaifa na Nukuu za Hamasa za Hayati baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere.
Katika kipengele cha Usalama,
Pasipoti hii ina kifaa maalum chenye uwezo wa kutunza taarifa za mmiliki wa
pasipoti “Micro Chip” na hivyo kufanya suala la utunzaji wa usalama wa pasipoti
hizi kuwa wa hali ya juu zaidi. Pasipoti hii ina uwezo wa kutunza kumbukumbu za
kibailojia (Biometric features). Pia
pasipoti hii ni ngumu kughushiwa na wahalifu au watu wanaojaribu kuficha
utambulisho wao kwa kutumia pasipoti zisizo zao.
Ikumbukwe kuwa,
Utekelezaji wa Mradi huu umefanyika kwa muda mfupi takribani miezi minne tangu
kusainiwa kwa mkataba na ukihusisha utoaji wa Pasipoti za aina tatu (Ordinary,
Service & Diplomatic)
Tuzo hiyo ilipokelewa na
Kamishna wa Uhamiaji (Pasipoti na Uraia) Gerald Kihinga kwa niaba ya Serikali
ya Tanzania na Idara ya Uhamiaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni